Mapenzi ya ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)

Usiku ule Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) anatoka kwenda kuhijiria kwenda Madinah Munawwarah, makafiri walikuwa wameizunguka nyumba yake ili wamuue.

Kabla ya kuondoka, Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alimuagiza ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kulala nyumbani kwake ili makafiri wafikirie kuwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) bado yuko ndani na hawatatambua kuwa alikuwa ameondoka.

Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alimjulisha ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Allah Ta’ala atamlinda na makafiri.

Wakati huu, licha ya hatari kubwa aliyokumbana nayo, ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa moyo wote alitekeleza maagizo ya Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam).

Kwa namna hii, ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa tayari kujitolea maisha yake mwenyewe kwa ajili ya kuokoa maisha ya baraka ya Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam).

Kuhusiana na hili, ‘Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akisoma mashairi yafuatayo:

Nilijitolea maisha yangu ili kulinda maisha ya mtu bora zaidi aliyewahi kukanyaga juu ya uso ya ardhi, na mtu bora kabisa aliyefanya tawaaf ya Ka’bah na Hajr-ul-Aswad.

(Huyu si mwingine ila) Mtume wa Allah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam), ambaye aliogopa vitimbi vya maadui zake kwake. Basi Allah Ta’ala, ambaye ndiye chanzo cha neema zote, akamuokoa na vitimbi vyao viovu.

Mtume wa Allah Ta’ala (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alikesha usiku mzima pale pangoni akiwa salama, akifurahia ulinzi wa Allah Ta‘ala na uficho.

Nilikesha usiku mzima nikiwatazama makafiri na hali hawakumtarajia mtu huyo (nyumbani kwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)) kuwa mimi (nimelala mahali pake), na nilikuwa nimejiweka tayari kufa au kutekwa.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …