Kipato Cha Rehema Kubwa Za Allah Subhaana Wata’alah

عن ابن عمر وأبي هريرة رضي الله عنهما قالا قال رسول الله صلى الله عليه وسلم صلوا علي صلى الله عليكم (الكامل لابن عدي، الرقم: ١١٠٨٦، وإسناده ضعيف كما في التيسير للمناوي ٢/٩٣)

Sayyidina Abdullah Bin Umar : (radhiyallahu ‘anhu) na Sayyidina Abu Hurairah : (radhiyallahu ‘anhu) wamesema kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “Tuma salaam kwangu, Allah subhaana wata’alah atakufariji na rehema”

Tamaa Ya Kuwa Pamoja na Rasulullah sallallahu alaihi wasallam

Siku moja, Sahaabi mmoja alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema: Ewe mjumbe wa Allah ta’ala wewe ni kipenzi kwangu kuliko maisha yangu, mali yangu na familia yangu. Nikiwa ndani ya nyumba yangu, naanza kukufikiria na kukosa utulivu. Kutotulia kwangu hakumaliziki mpaka macho yangu ikushuhudie. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), kifo hakiepukiki. Baada ya kufa, utakuwa katika hali ya juu, iliyotukuka cheo kama wewe ni Nabii na Mtume wa Allah ta’ala, hali mimi nitakuwa mbali nawe. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), labda sitopata baraka ya kukuona. Kila nikiwaza haya
utengano kati yetu ambao utasababishwa na kifo, nakuwa na huzuni nyingi.”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alinyamaza juu ya hili mpaka Jibreel (alahis salaam) alishuka na aya ifuatayo ya Quran Tukufu:

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَ وَحَسُنَ أُو۟لَٰٓئِكَ رَفِيقًا

Watu wote wanaomtii Allah ta’ala na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wamo katika kundi la wale ambao juu yao ziko rehema za Allah ta’ala; Manabii (alahimus salaam), Siddiqin, Mashahidi, na Wachamungu.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …