Sunna na Adabu

Sunna za Msikiti

25. Usipasue vifundo vyako ukiwa msikitini. Vile vile, usiunganishe vidole vyako ukiwa umeketi msikitini.

Mtumwa aliyeachiliwa huru wa Sayyidina Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Siku moja, nikiwa na Abu Sa’eedd (radhiyallahu ‘anhu) na yeye akiwa pamoja na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), tuliingia msikitini na tukamuona mtu mmoja ameketi katikati ya musjid. Mtu huyu alikuwa amekaa kitako kwa jinsi magoti yake yalivyoinuliwa, na mikono yake ikiwa imezunguka magoti yake, na vidole vya mikono yake yote miwili vimeunganishwa. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliimpa ishara mtu huyu (kuvuta mazingatio yake), lakini mtu huyo hakuona ishara ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hivyo akageuka kumelekea Abu Sa’eed (radhiyallahu ‘anhu) na akasema, ‘Mmoja wenu atakapokuwa msikitini, basi asiunganishe vidole vyake, kwani kuunganisha vidole vyake ni kutoka kwa Shetani. Kwa muda utabakia msikitini mkingojea Swalaah, mtapata ujira wa Swalaah kama mko katika Swalaah mpaka mtakapotoka msikitini. Kuunganisha vidole wakati wa Swalaah ni kinyume na adabu ya Swalaah, basi mtu hatakiwi kuunganisha vidole wakati wa kusubiri Swalaah).’”

Soma Zaidi »

Sunna za Msikiti

21. Usipite mbele ya mtu anayeswali. Lakini, ikiwa ameweka sutrah mbele yake (yaani kuweka kitu chochote kirefu ili watu wapite mbele yake), inajuzu kupita mbele ya sutrah.[1] عن أبي جهيم رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لو يعلم المار بين يدي المصلي ماذا عليه لكان …

Soma Zaidi »

Sunna za Msikiti

18. Ni bora mtu asiutumie msikiti kama njia ya kupita (kupitia ng’ambo).[1] عن ابن عمر رضي الله عنهما عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال خصال لا تنبغي في المسجد لا يتخذ طريقا ولا يشهر فيه سلاح (سنن ابن ماجة، الرقم: 748)[2] Sayyidina Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Sayyidina …

Soma Zaidi »

Sunna Za Msikiti

14. Hakikisha unazima simu yako ya mkononi unapoingia msikitini ili isilete usumbufu kwa wale wenye
kujishughulisha na kuswali na ibaadaah zingine.

15. Usipige picha au kutengeneza video ukiwa msikitini. Kupiga picha au kutengeneza video za vitu vilivyo hai ni haraam katika Uislamu, na kufanya hivyo katika msikitini ni dhambi kubwa zaidi.

Soma Zaidi »

Sunna Za Msikiti.

13. Usipaze sauti yako au kufanya kelele ndani ya msikiti na katika eneo linalozunguka musjid.[1] عن السائب بن يزيد رضي الله عنه قال كنت نائما في المسجد فحصبني رجل فنظرت فإذا عمر بن الخطاب رضي الله عنه فقال اذهب فأتني بهذين فجئته بهما فقال ممن أنتما أو من أين أنتما …

Soma Zaidi »

Sunna Za Msikitini

9. Fanya niya ya nafil i'tikaaf kwa ajili ya kuwa utakaa msikitini.

10. Swali rakaa mbili za tahiyyatul masjid ukiingia msikitini.

Sayyidina Abu Qataadah (radhiyallahu ‘anhu) amesema kuwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, "pindi mmoja wenu atakapo ingia msikitini, anatakiwa kuswali rakaa mbili za swala kabla ya kukaa,"

Soma Zaidi »

Sunna na Adabu za Kuchinja – Sehemu ya 3-

11. Ikiwa mtu ana uwezo, ni bora kwake kuchinja mnyama mwenyewe. Ikiwa hili haliwezekani, basi angalau ashuhudie mnyama wake akichinjwa, mradi tu hijaab inazingatiwa kati ya wanaume na wanawake (yaani kuingiliana kusifanyike). عن علي رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال يا فاطمة قومي فاشهدي …

Soma Zaidi »