12. Unapozungumzia kuhusu Qur’an, basi ipe cheo cha heshima kama vile Quraan Majeed, Quraan Kareem, Quraan Tukufu, Quraan Takatifu, n.k.
13. Soma Quran Majeed kwa sauti nzuri. Vile vile, unapaswa kujiepusha na kuiga sauti na urembaji wa nyimbo na mitindo ya waimbaji, nk.[1]
Baraa ibn Aazib (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Ipendezesheni (usomaji wako) Qur’an Tukufu kupitia sauti zenu (kwa kuisoma kwa sauti nzuri).”[2]
Hudhaifa (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Soma Quran tukufu kwa sauti na mitindo ya Waarabu, na mjiepushe na (kukariri) mitindo ya Ahlul Kitaab na mitindo ya watu waovu. Hivi karibuni baada yangu, watu watakuja ambao watasoma Quran Majeed kwa mtindo ya waimbaji, watakuwa kama watu wanaoomboleza. Kisomo chao hakito pita hata koromeo zao (yaani hakitapanda na kwenda kwa Allah Ta’ala na hakito kubaliwa, kwa sababu ya wao kuisoma kwa namna isivyo sahihi, au haitafika kwenye nyoyo zao na kuathiri nyoyo zao), zitadhurika nyoyo zao na nyoyo za waliyo radhi nao. (kwa kuipenda dunia).[3]
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Yeye si miongoni mwetu asiyesoma Qur’an Takatifu kwa sauti nzuri.[4]
14. Unapojishughulisha na usomaji wa Quraan Majeed, unapaswa kuonyesha umakini wako kamili kwa Quraan Takatifu. Hupaswi kujihusisha na mijadala ya kidunia kati ya usomaji wako, hasa pale pindi Quraan Takatifu inapoachwa wazi. Iwapo kuna haja ya wewe kuzungumza, basi unatakiwa kukamilisha Aayah unayosoma, ufunge Qur’an Takatifu kwa heshima, na baada ya hapo uongee.
Imepokewa kwamba wakati wowote Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhu) alipokuwa akisoma Quran Takatifu, alikuwa hajishughulishi na mjadala wowote (wa kidunia) mpaka amalize kusoma.[5]
[1] وقراءة القرآن بالترجيع قيل لا تكره وقال أكثر المشايخ تكره ولا تحل لأن فيه تشبها بفعل الفسقة حال فسقهم ولا يظن أحد أن المراد بالترجيع المختلف المذكور اللحن لأن اللحن حرام بلا خلاف (الفتاوى الهندية 5/317)
[2] سنن أبي داود، الرقم: 1468، وقال الحافظ في فتح الباري 13/519 : قوله وزينوا القرآن بأصواتكم هذا الحديث من الأحاديث التي علقها البخاري ولم يصلها في موضع آخر من كتابه وقد أخرجه في كتاب خلق أفعال العباد من رواية عبد الرحمن بن عوسجة عن البراء بهذا وأخرجه أحمد وأبو داود والنسائي وابن ماجة والدارمي وابن خزيمة وابن حبان في صحيحيهما من هذا الوجه وفي الباب عن أبي هريرة أخرجه ابن حبان في صحيحه وعن ابن عباس أخرجه الدارقطني في الأفراد بسند حسن
[3] المعجم الأوسط للطبراني، الرقم: 7223 وقال الحافظ في نتائج الأفكار 3/223: هذا حديث غريب أخرجه أبو عبيد عن نعيم بن حماد عن بقية وأخرجه أبو أحمد الحاكم في الكنى عن أحمد بن عبد الرحمن بن خلاد عن محمد بن مهران فوقع لنا بدلاً عالياً في الطريقين أخرجه ابن عدي عن الحسين بن عبد الله القطان عن سعيد بن عمرو عن بقية قال الطبراني لا يروى عن حذيفة إلا بهذا الإسناد تفرد به بقية قلت وهو مشهور بالتدليس عن الضعفاء والمجهولين وما روى عن شيخه حصين أحد غيره وشيخه أبو محمد لا يعرف اسمه ولا له إلا هذا الحديث
[4] صحيح البخاري، الرقم: 7527
[5] صحيح البخاري، الرقم: 4526