Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) akitoa Adhaan ndani ya Shaam

Wakati mmoja pindi ‘Umar (Radhiyallahu’ Anhu) alisafiri kwenda Baitul Muqaddas wakati wa Khilafa yake, alitembelea Jaabiyah (sehemu mmoja ndani ya Shaam). Wakati alikuwa ndani ya Jaabiyah, watu walimwendea na kumuuliza ikiwa angemuomba Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu), ambaye alikuwa akiishi Shaam, awatolee adhaan, kwa sababu yeye alikuwa Muadhin wa Rasulullah (Sallallahu Alaihi Wasallam) Madina Munawwarah.

‘Umar (Radhiyallahu’ Anhu) alimuomba Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) atowe adhaan na mara moja akakubali.

Mara tu Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alipoanza kutoa Adhaan, watu walikumbushwa na enzi ya baraka wa Rasulullah (Sallallahu Alaihi Wasallam) pindi Bilaal (Radhiyallahu’ Anhu) alikuwa akitoa adhaan huko Madinah. Hii ilisababisha walie kwa huzuni kwa sababu Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alikuwa hayuko tena duniani.

Akielezea kiwango cha huzuni ya watu, Aslam (Rahimahullah), mtumwa aliyeachiliwa huru wa ‘Umar (Radhiyallahu’ Anhu), alisema, “Sijawahi kuona watu wakilia siku yoyote kuliko vile nilivyowaona wakilia siku hiyo.” (Siyar A’laamin Nubalaa 3/222, Sharhuz Zarqaani 5/71)

About admin

Check Also

Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) Akitoa Adhaan Juu Ya Ka’bah Shareef

Katika hafla ya Fath-ul-Makkah (ushindi wa Makkah), Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) aliingia ndani ya Ka’bah …