Sunnah na Adabu Za Kusoma Qur’an Takatifu 3

9. Soma ta’awwudh (a’uudhu billah) unapoanza kusoma Quran Takatifu.

فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ‎﴿٩٨﴾

Unapokusudia kusoma Quran, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu na Shetani, aliyekataliwa.[1]

10. Unapaswa kusoma Qur’an Takatifu wakati moyo wako uko makini kwenye kusoma. Ikiwa unahisi uchovu na unaona kuwa uzingatio wako umeathiriwa, basi unapaswa kuacha kusoma na kuendelea wakati unaweza kuzingatia na kuwa makini zaidi.

Jundub bin Abdillah (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Rasulullah (Sallallahu’alaihi wasallam) amesema: “Someni Qur’an kama tu nyoyo zenu zipo makini (kuelekea kusoma Quraan Takatifu), na mnapo poteza mwelekeo (kwa kuchoka na kughafilika), basi acheni kusoma.[2]

11. Soma Quran Takatifu kwa tajweed na kwa matamshi sahihi. Hata kama unasoma Qur’an Takatifu kwa mwendo wa haraka, unapaswa kuhakikisha kwamba unasoma kila neno kwa uwazi kwa tajweed na matamshi sahihi.[3]

وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا ‎﴿٤﴾

Na soma Qur’an Takatifu kwa tarteel (kwa utaratibu na sauti).[4]

Imepokewa kwamba katika tukio moja, mtu mmoja alikuja kwa Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akataja, “Ninasoma Sura zote za Mufassal (yaani kutoka Surah Hujurat mpaka mwisho wa Quran Takatifu) ndani ya rakaa moja.” Aliposikia haya, Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “(wenda kusoma kwako ni kwa haraka) kama usomaji haraka wa mashairi (yaani usomaji wako ni wa haraka na bila tajweed, kama jinsi mashairi wakisoma haraka). Hakika baadhi ya watu watasoma Qur’an Takatifu, lakini haitapita koo zao (yaani haitapanda kwa Allah Ta’ala na kukubaliwa kwa sababu ya wao kuisoma vibaya, au haitazifikia nyoyo zao na kuathiri nyoyo zao).[5]


[1] سورة النحل: 98

[2] صحيح البخاري، الرقم: 5061

(وعن جندب) بضم الجيم والدال ويفتح (ابن عبد الله قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: اقرءوا القرآن ما ائتلفت عليه قلوبكم) أي ما دامت قلوبكم وخواطركم مجموعة لذوق قراءته ذات نشاط وسرور على تلاوته (فإذا اختلفتم) أي اختلفت قلوبكم ومللتم وتفرقت خواطركم وكسلتم (فقوموا عنه) أي فاتركوه (مرقاة المفاتيح 4/1496)

[3] والأخذ بالتجويد حتم لازم … من لم يجود القرآن آثم

لأنه به الإله أنزلا … وهكذا منه إلينا وصلا (المقدمة الجزرية صـ ١١)

[4] سورة المزمل: 4

[5] صحيح مسلم، الرقم: 1860

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …