15. Ikiwa unaswali rakaa tatu au nne, basi katika rakaa ya tatu na ya nne utasoma tu Surah Faatihah. Hupaswi kusoma surah yoyote baada ya kusoma Surah Faatihah.
Kumbuka: Katika rakaa ya tatu na ya nne kwenye swala ya fardh, Surah Faatihah itasomwa na imaam, muqtadi (mfwasi nyuma ya imaam) na munfarid (mwenye kuswali peke yake).
Katika rakaa zote za sunnah na swala za nafl, surah fatihah na surah nyingine yoyote itasomwa.