Istiqaama wa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) juu ya Uislamu:

Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) ni Sahaabi maarufu kati maswahaabah (Radhiyallahu’ Anhum), na alikuwa Muazzin wa msikiti wa Mtume (Sallallahu ‘Alaihi wasallam) . Mwanzoni alikuwa mtumwa wa Abyssinia wa kafiri mmoja huko Makkah Mukarramah. Yeye kuwa muislamu, kama kawaida, haukupendwa na mmiliki wake na kwa hivyo aliteswa bila huruma.

Ummayah bin Khalaf, ambaye alikuwa adui mkubwa zaidi wa Uisilamu, alikuwa akimfanya alale juu ya mchanga unaonguza na ukali wa juwa mchana na akiweka jiwe nzito kwenye kifuwa chake, ili asiweze hata kutikisa mwili wake. Kisha alikuwa akimwambia, “Acha Uislamu, au teseka na ufe.”

Hata katika hali hii, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alikuwa akisema, “Ahad! (Mwenyezi Mungu mmoja!) Ahad! (Mwenyezi Mungu mmoja!)”

Usiku, alikuwa akifungwa na minyororo na kuchapwa, na sehemu ambapo alikuwa amechanika alikuwa akilazwa chini kwenye mchanga wenye moto uliowaka mchana ili aache Uisilamu au kufa kifo cha maumivu wa majeraha. Wanyanyasaji walikuwa wakichoka na kuchukua zamu. Wakati mwingine, Abu Jahl angemtesa, wakati mwingine, Umayyah au mtu mwingine angekamilisha adhabu hiyo, na wakishindana na mwenzake kwa kumtesa na adhabu kali na chungu zaidi, lakini Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alikuwa hatowi hata sauti kwa kulalamika.

Kuona mateso mabaya ambayo Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alikuwa akipitia, Abu Bakr (Radhiyallahu’ Anhu) alimnunua na kumwacha huru, na akawa Mwislamu huru.

Kama vile Uislam unavyofundisha umoja wa Allah Ta’ala, wakati waabudu sanamu wa Makka Mukarramah waliamini masamu mengi, kwa hivyo Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alirudia neno, “Ahad! (Mwenyezi Mungu mmoja!) Ahad! (Mwenyezi Mungu mmoja!)” Hii inaonyesha upendo wake wa dhaati kwa Allah Ta’ala (Al Isaabah 1/456, Fadhaa’il-ul-A’maal pg. 21-22,)

About admin

Check Also

Heshima ya Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu ‘Anhu) kwa Uthmaan (Radhiyallahu’ Anhu)

Inaripotiwa kuwa katika hafla moja, mtu alifika kwa Sa’eed bin Zaid (Radhiyallahu ‘Anhu) na akasema, …