Qiyaam

10. Mara tu unapoanza swalah yako, soma Dua-ul- Istiftah kimya kimya:

وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِيْ فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيْفًا مُسْلِمًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِيْنَ إِنَّ صَلَاتِيْ وَنُسُكِيْ وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِيْ لله ِرَبِّ الْعَالِمِيْنَ لَا شَرِيْكَ لَهُ وَبِذلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِيْنَ

Nauelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, huku nikiwa nimekaa kwenye njia iliyonyooka bila ya upotovu wowote, kwa utiifu, na mimi si miongoni mwa wanaomshirikisha Allah Ta’ala. Hakika Swalaah yangu, ibada zangu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah Ta’ala, Mola wa ulimwengu wote. Hana mshirika, na haya ndiyo niliyoamrishwa nayo, na mimi ni miongoni mwa waliosilisha (kwa Allah Ta’ala).

11. Soma Ta’awwudh. Ta’awwudh ni kusoma:

أَعُوْذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيْم

Najikinga kwa Allah Ta’ala na shetani aliyelaaniwa.

12. Baada ya hapo somo la Surah Faatihah ikifuatiwa na surah au sehemu yoyote ya Quraan Takatifu. Kabla ya kuanza kusoma surah faathihah, soma tasmiyah kwa sababu ni sehemu pia ya surah fatihah.

Tasmiyah ni kusoma:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيْم

Kwa jina la Allah Ta’ala, mwingi wa upendo, mwingi wa rehema.

Kumbuka: Wanawake hawatakiwi kuswali kwa sauti. Wanatakiwa kutekeleza kila Swalah kimyakimya.

13. Soma “ameen” baada ya Surah Fatihah.

14. Soma tasmiyah kabla ya surah.

Kumbuka: Tasmiyah itasomwa tu (baada ya Surah Faatihah) ikiwa mtu ataanza kusoma mwanzo wa surah. Ikiwa mtu hataanza mwanzo wa Sura yoyote basi tasmiyah isisomwe.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo …