Fikra Ya Umar (radhiyallahu ‘anhu) kwa ajili ya Swalaah

Asubuhi ambao Umar (radhiya allaahu ‘anhu) alichomwa kisu, Miswar bin Makhramah (radhiyallahu ‘anhu) alikuja kumuona. Alipoingia, alimkuta Umar (radhiya allaahu ‘anhu) amefunikwa akiwa na karatasi na kupoteza fahamu.

Miswar (radhiya allaahu ‘anhu) akawauliza wale waliokuwepo pale, “yukoje?” Wakajibu, “Hana fahamu kama unavyoona.” Kwa vile kulikuwa hakuna muda mwingi uliobakia kwa ajili ya Swalah ya Alfajri, Miswar (radhiya allaahu ‘anhu) akawausia, “Mwamsheni kwa kumuita kwa ajili ya Swalaah, kwa sababu hakuna chochote mnachoweza kumuamsha chene dharura na muhimu zaidi kwake kuliko Swalaah.”

Hivyo wakasema: “Swalaah, ewe Ameer-ul-Mu’mineen! Mara tu walipofanya hivi, Umar (radhiyallahu ‘anhu) aliamka na kusema, “Ndiyo! Wallahi! Hakuna sehemu na nafasi ndani ya Uislamu kwa yule ambaye anapuuza swalah!”

Umar (radhiya allaahu ‘anhu) baada ya hapo aliswali huku damu ikitoka kwenye donda lake. (Al-Mu’jamul Awsat #8181)

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …