Ruku na I’tidaal

7. Soma tasbeeh ifuatayo mara tatu au idadi yoyote isiyo ya kugawanyika:

سُبْحَانَ رَبِّيَ الْعَظِيْم

Utukufu ni wa Mola wangu Mkubwa.

8. Baada ya kusoma tasbihi, simama kutoka kwenye rukuu huku ukisema tasmee’:

سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهْ

Allah Ta’ala Humsikia mwenye kumsifu.

9. Inua mikono (kama ilivyoelezwa katika takbeeratul ihraam) na iweke pembeni.

10. Soma Tahmid:

رَبَّنَا لَكَ الْحَمْد

Ewe Mola wetu, hakika kwako wewe pekee ndiyo sifa njema.

11. Simama wima kwa tumaaninah (mwili upate utulivu kabisa) kabla ya kuingia kwenye sajdah.

About admin

Check Also

Qa’dah Na Salaam

7. Ikiwa ni qa’dah ya mwisho, basi soma tashahhud, Swalawaat Ebrahimiyyah na baada ya hapo …