Matamanio Ya Umar (radhiya allaahu ‘anhu) Kuzikwa Pamoja Na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

 

Katika dakika za mwisho baada ya Umar (radhiya allaahu ‘anhu) kuuawa kwa kuchomwa kisu, alimtuma mwanawe, Abdullah bin Umar (radhiya allaahu ‘anhuma), nyumbani kwa Aaishah (radhiyallahu ‘anha).

Umar (radhiya Allaahu ‘anhu) alimuagiza akisema, “Mwambie kwamba Umar anatoa salaam. Usiseme kwamba Ameer-ul-Mu’mineen anafikisha salaam, kwa sababu leo mimi sio Amirul-Mu’mineen tena (kama ninavyokaribia kufariki). Mwambie kwamba Umar bin Khattaab anaomba ruhusa ya kuzikwa pamoja na masahaba wake wawili, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhu)).

Kufuatia maagizo ya baba yake, Abdullah bin Umar (radhiya allaahu ‘anhuma) alikwenda nyumbani kwa Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) ambapo alimkuta amekaa na akilia (kwa msiba huu mkubwa na hasara ambayo umma ungeupata kupitia kufariki kwa Umar (radhiyallahu ‘anhu)).

Akamfikishia salamu ya Umar (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akasema: “Umar anaomba ruhusa azikwe pamoja na masahaba wake wawili.” Kusikia ombi hilo, Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) akasema, “Nilikuwa nikitarajia kuzikwa hapo (karibu na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), na baba yangu, Abu Bakr (Radhiyallahu ‘anhu)). Lakini, leo nitatoa upendeleo kwa Umar
(radhiya allaahu ‘anhu) juu yangu.”

Aliporudi Abdullah bin Umar (radhiya allaahu ‘anhuma) na akamtaja Umar (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) ametoa ruhusa azikwe pamoja na Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) na Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu), Umar (radhiyallahu ‘anhu) alifurahishwa sana.

Kisha Umar (radhiya allaahu ‘anhu) alimuagiza zaidi mwanawe Abdullah bin Umar (radhiya allaahu ‘anhuma) akisema, “Baada ya mimi kufa, unapoubeba mwili wangu kwenye maziko, basi muulize tena Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) ruhusa kwa niaba yangu ukisema, ”Umar anaomba ruhusa kuzikwa pamoja na wenzake wawili.”Ikiwa atatoa ruhusa tena, basi nizike huko. Kama sivyo basi nizike kwenye makaburi ya Waislamu ya kawaida.” (Swahih Bukhaari #3700)

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …