Sunnah na Adabu Za Kusoma Qur’an Takatifu 5

15. Wakati wa kugeuza kurasa za Qur’an Takatifu, usiloweshe kidole chako na mate ili kugeuza kurasa. Hii haiendani na heshima tunayotakiwa kuionyesha Quraan Majeed.

16. Baada ya kuhitimisha Quraan Takatifu, unapaswa kushiriki katika dua kwa sababu huu ni wakati ambao dua zinakubaliwa.

Thaabit (rahimahullah) anaripoti kwamba wakati wowote Anas bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) alikua akihitimu Qur-aan Takatifu, alikuwa akiikusanya familia yake na watoto wake na kisha kuwafanyia dua.

Ibrahim Taimi (rahimahullah) amesimulia kwamba Abdullah bin Mas’ud (radhiyallahu ‘anhu) alisema, “Yoyote anayemaliza kisomo kamili cha Qur-aan Majeed basi (aombe dua) dua yake itakubaliwa,” Ibrahim Taimi (rahimahullah) baadaye alitaja kwamba wakati wowote Abdullah bin Mas’ud anapokamilisha Qur’an Tukufu, basi alikuwa akiikusanya familia yake na kushiriki katika dua, na walikuwa wakisema Aamin kwenye dua yake.

Humaid (rahimahullah) amesema: “Mwenye kusoma Quran Takatifu na kisha akaomba dua, Malaika elfu nne husema Amin kwenye dua yake.

17. Haijuzu kwa mwenye hali ya janaaba au mwanamke aliye katika hali ya haidh kusoma Quraan Takatifu. Lakini, inajuzu kwao kusoma Aaya katika Quraan Takatifu ambazo ni dua kwa Allah Ta’ala pamoja na zile Aaya zinazosomwa kwa ajili ya kujikinga na mashetani, maovu n.k. Wanapozisoma hizi aaya wanatakiwa kuzisoma pamoja na niyyah ya dua na isti’aazah (kutafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Wasizisome na niyyah ya tilaawa (kisomo).

Ibnu Umar (radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mtu katika hali ya Haidh au Janaabah hatakiwi kusoma sehemu yoyote ya Quraan Takatifu.


 

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 1

1. Unapokutana na ndugu yako Muislamu, muamkie kwa kutoa salaam. Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaripoti …