Sunnah na Adabu Za Kusoma Qur’an Takatifu 6

18. Haijuzu kwa mtu kusoma sehemu yoyote ya Quraan Takatifu au kuchukua jina la Allah Ta’ala akiwa chooni. Vile vile ikiwa mtu ana pete au cheni ambayo juu yake imeandikwa jina la Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) au aya yoyote ya Quraan Majeed, basi aiondoe kabla ya kuingia chooni.

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akiivua pete yake pindi alipoingia chooni. (kwa sababu ilikuwa na jina la Allah Ta’ala).

19. Ikiwa unataka kubadilisha nguo zako chumbani ambapo kuna Quran Takatifu imetunzwa, basi unatakiwa uweke Qur’an Takatifu kwenye kabati kabla ya kuvua nguo. Kuvua nguo mbele ya Quran Takatifu ni kinyume na heshima ya Quran Majeed.

20. Ukisoma Aayah ya Sajdah au ukiisikiliza pindi inaposomwa, basi ni waajib (lazima) juu yako kusujudu. Namna ya kufanya sajdah-tu-tilaawa ni utasema takbira na kwenda katika mkao wa sajdah. Baada ya hapo, utasema takbira tena na utainuka kutoka sajdah. Ni mustahab kufanya sajdah kutokea mkao wa kusimama.

Lakini, ikiwa hili ni gumu, basi inajuzu kufanya sajdah kutoka katika mkao wa kukaa.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Wakati mtoto wa Aadam (‘alaihis salaam) anaposoma aaya ya sajdah kisha akafanya sajdah, shetani husogea huku analia, akisema, ‘Maangamizo kwangu! Mtoto wa Aadam (‘alaihis salaam) aliamrishwa kusujudu na akasujudu, kwa hiyo atapata Jannah. Mimi niliamrishwa nifanye sajdah na nikakataa, kwa hiyo nitapata moto wa Jahannum.”

21. Unapomaliza tilaawa ya Quraan Takatifu (yaani kuhitimu) yote na kufika Surah Naas, basi ni mustahab kwako kuanza tena Quraan Takatifu kwa kusoma Surah Faatihah na aya za mwanzo za Surah Baqarah mpaka اَلمفْلِحُون.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …