Malaika sabini wanarikodi thawabu kwa siku elfu moja

Sayyidina ibn Abbaas (radhiyallahu ‘anhuma) anasimulia kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, "Yoyote atakayenitumia salaam ifuatayo, (akajishughulisha na) akawachosha malaika sabini (katika kurikodi thawabu ya salaam iliyosomwa) kwa siku elfu moja."

Allah subhaana wata'ala amlipe Nabii Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa niaba yetu kama anavyostahili (yaani: thawabu inayostahili nafasi yake tukufu).

Soma Zaidi »

Muharram na Aashura

Ni mfumo wa Allah ambao ametoa wema maalum na umuhimu kwa baadhi ya mambo juu ya mengine. kutoka kwa wanadamu, manabii wamebarikiwa na vyeo na hali ya juu ya wengine. kutoka sehemu tofauti ulimwenguni haramain shareefain (Makka mukarrama na madina munawwara) na musjid Alaqsa wamepewa daraja maalum juu ya ulimwengu …

Soma Zaidi »

Mahitaji Ya Dunia Na Ya Aakhera Kutimizwa Kwa Kumsalia Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Siku Ya Ijumaa

Sayyidina Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, wale miongoni mwenu wanao niswalia zaidi duniani watakuwa karibu na mimi siku ya qiyamah, kila wakati. Yoyote ambaye ananiswalia usiku wa ijumaa na mchana wa ijumaa, Allah subhaana wata'alah atatimiza haja zake mia moja, mahitaji sabini ni aakhera na mahitaji thelathini ni ya duniani. baada ya kuniswalia, Allah subhaana wata'alah atamkabidhi malaika ambaye ataniletea kaburini, kama vile zawadi imeletwa kwako. Malaika wananijulisha mtu aliye niswalia kwa kuniambia jina lake na family yake. Kisha natunza salaam kwangu kwenye kitabu cheupe.

Soma Zaidi »

Kupata Maombezi Ya Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن رويفع بن ثابت قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى على محمد وقال: اللهم أنزله المقعد المقرب عندك يوم القيامة، وجبت له شفاعتي (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: ٤٤٨٠، وإسناده حسن كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٣٠٤) Sayyidina Ruwaifi Bin Thaabit Al ansaari (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba …

Soma Zaidi »

Kutokomeza Kwa Umasikini

Sayyidina Samurah Suwaai (radhiallahu anhu), baba wa Sayyidina Jaabir (radhiallahu anhu), ameripoti kwamba: tuliwahi kuwa na Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) pindi mtu mmoja alikuja kwa Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na akauliza, " ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) !ni tendo gani linalomrizisha Allah subhaana wata'alah zaidi?" Nabii wa Allah-(sallallahu alaihi wasallam) akajibu, "maneno ya ukweli na kutimiza uwaminifu." Nikasema, "ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha (kuhusu matendo yanayo mrizisha Allah subhaana wata'alah)!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " swali wakati wa usiku na funga wakati wa jua kali." Kisha nikasema, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha!" Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, " jishughulishe na zikr kwa wingi na nitumie salaam inaondowa umasikini," nikauliza tena, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) nakuomba utuzidishie nasaha! Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, yule atakae  swalisha  watu basi  afupishe swala,kwa sababu kwenye jamaa  kuna wazee, kuna wagonjwa, vijana na watu kuna ambao wana dharura."

Soma Zaidi »