Sayyidina Abdullah Bin Mas'ood (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah(sallallahu 'alaihi wassallam) amesema "mtu ambaye atake kuwa karibu sana na mimi (ambae anastahili sana msamaha wangu) siku ya kiama ni yule ambae alikuwa ananiswalia sana duniani."
Soma Zaidi »Kupata Qiraat Moja Ya Thawabu
Sayyidina Ally Bin Abii Taalib (radhiyallahu 'anhu) anaripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema, "yoyote atakae niswalia mara moja, Allah subhaana wata'alah atamuandikia kirati moja ya thawabu, na kirati moja ni sawa na mlima wa uhudi.
Soma Zaidi »Kupata Thawabu Sabini
Sayyidina Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu 'anhuma) alitowa ripoti, "Yoyote atakaye tuma salaam kwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) mara moja Allah subhaana wata'alah na malaika wake watatuma sabini rehema na baraka juu yake kwa kulipa salaam moja yake. Kwahivyo yoyote atakaye taka kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) azidishe kumsaliya Nabii. Na yoyote atakaye kuwa ataki kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) asizidishe kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) (yaani kama anataka kupata ujira mwingi,ni lazima azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam)).
Soma Zaidi »Kupata Rehma Kubwa Za Allah Subhaana Wata’alah
Sayyidina Abdullah Bin Umar : (radhiyallahu 'anhu) na Sayyidina Abu Hurairah : (radhiyallahu 'anhu) wamesema kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema, "Tuma salaam kwangu, Allah subhaana wata'alah atakufariji na rehema"
Soma Zaidi »Kupata Rehma Kumi
Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema " yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata'alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi"
Soma Zaidi »Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaanahu Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)
Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa.
Soma Zaidi »Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili
4. Osha mikono yote mpaka kwenye vifundo mara tatu
Sayyidina Humraan (rahimahullah), mtumwa aliye huru wa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu)aliomba aletewe maji (kuonyesha watu jinsi gani ya kuchukuwa udhu). Kisha alianza kutawadha kwa kuosha mikono (mpaka kwenye vifundo) mara tatu. (kwenye riwaya hii, iliyopatikana ndani ya Sahihi Bukhari, Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kasema ” nilimuona Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) anafanya udhu kwa namna hii.)”
Soma Zaidi »Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Kwanza
1. Pindi hukifanya udhu, elekea qibla na kaa sehemu ya juu ( mf: kiti) ili usipatwe na maji yaliyotumika. Sehemu ambayo mtu anafanya udhu iwe safi.
Sayyidina Abd kheir (rahimahullah) ameripoti kwamba kiti kililetwa kwa Sayyidina Ally (radhiyallahu ‘anhu). Kisha aka kaa juu ya kiti ( kwa ajili ya kuonyesha udhu wa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam).
Soma Zaidi »Masaili Ya Kawaida Yanayohusiana Na Kujisaidia Mwenyewe
1. S: Je inaruhusiwa kusoma kitu chochote kilichoandikwa kwa mfano magazet,kutumia simu kuchat, kutumia internet, na mengineyo wakati uko chooni ?
J: Chooni ni sehemu ambayo mtu anajisaidia, hivyo haipendezi kwa mtu kutumia simu yake au kusoma kitu chochote chenye maandishi chooni.[1]
Soma Zaidi »Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya saba
22. Pindi ukitumia choo Usikiache katika hali ya uchafu mf: kuchafua juu ya choo au kuchafua chini, kwa kutofurashi na maji nk:kama unatumia choo ambacho kinatumiwa na watu wengine kuwa makini zaidi kwa utumiaji wako ili usilete usumbufu kwao
Soma Zaidi »