18. Mtu asianze kumchuna mnyama huyo mpaka kusiwe na dalili ya uhai iliyosalia katika mwili.
19. Wakati wa kuchinja mtu asome tasmiyah kwa namna ifuatayo:
بِسمِ اللهِ اللهُ أكْبَر
Kwa jina la Allah Ta’ala, na Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi.
20. Kabla ya kuchinja ni sunna kwa mtu kusoma dua ifuatayo:
إنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ عَلَى مِلَّةِ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
إنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ اللهُمَّ مِنكَ وَ لَكَ
Nimejielekeza kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, na mimi niko kwenye Dini Iliyo Nyooka ya Ibrahim, na mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika Swalah yangu, na kafara yangu, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah Ta’ala, Mola wa ulimwengu wote. Hana mshirika, kwa hili nimeamrishwa na mimi ni miongoni mwa Waislamu. Ewe Allah! Sadaka hii inatokana na Wewe kutupa uwezo wa kufanya hivyo na ni kwa ajili Yako.
عن جابر بن عبد الله رضي الله عنه قال ذبح النبى صلى الله عليه وسلم يوم الذبح كبشين أقرنين أملحين موجئين فلما وجههما قال إنى وجهت وجهى للذى فطر السموات والأرض على ملة إبراهيم حنيفا وما أنا من المشركين إن صلاتى ونسكى ومحياى ومماتى لله رب العالمين لا شريك له وبذلك أمرت وأنا من المسلمين اللهم منك ولك عن محمد وأمته باسم الله والله أكبر ثم ذبح. (سنن أبي داود، الرقم: 2797)
Jaabir (radhiallahu anhu) anaripoti kwamba siku ya kuchinja, Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alichinja kondoo wawili mweusi na mweupe, wenye pembe, waliohasiwa. Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alipowaweka chini ili kuwachinja, alisoma dua ifuatayo:
إنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
إنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ اللهُمَّ مِنكَ وَ لَكَ
21. Imeandikwa katika Hadith kwamba kitendo bora kabisa kinachofanywa siku ya kuchinja (kutoka kwenye ibaada za muhimu) ni kumwagika kwa damu. Kwa hivyo, Rasulullah (Sallallaahu alayhi wasallam) ameeleza kuwa kitendo kitakachomletea mtu malipo makubwa zaidi ni kujiunga na mahusiano ya kifamilia ambayo yamekatika. Hivyo, pamoja na kutekeleza wajibu wa uchinjaji, tunapaswa kuhakikisha tunajiunga na kudumisha mahusiano ya kifamilia.
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم في يوم أضحى ما عمل آدمي في هذا اليوم أفضل من دم يهراق إلا أن يكون رحما مقطوعة توصل (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 10948)
Imepokewa kutoka kwa ibnu Abbaas (Radhiallaahu anhu) kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alayhi wasallam) alisema katika siku ya Eidul Adha (idi kubwa): “Hakuna kitendo chochote anachofanya mja katika siku hii ambacho ni kheri zaidi kuliko kumwagika kwa damu (kuchinja) ispokuwa kwa yule anayeunga na mahusiano ya familia ambayo yametengwa.”