Salaa na Salaam Maalum ya Ibnu Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu)

عن عبد الله بن مسعود قال: إذا صليتم على رسول الله صلى الله عليه وسلم فأحسنوا الصلاة عليه فإنكم لا تدرون لعل ذلك يعرض عليه قال: فقالوا له: فعلمنا قال: قولوا: اللهم اجعل صلواتك ورحمتك وبركاتك على سيد المرسلين وإمام المتقين وخاتم النبيين محمد عبدك ورسولك إمام الخير وقائد الخير ورسول الرحمة اللهم ابعثه مقاما محمودا يغبطه به الأولون والآخرون اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وآل إبراهيم إنك حميد مجيد اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وآل إبراهيم إنك حميد مجيد (سنن ابن ماجة، الرقم: 906، وإسناده حسن كما في الترغيب و الترهيب، الرقم: 2588)

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) Anaeleza, “Unapomswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), basi mswalie kwa adabu bora zaidi (yaani kwa kujitolea, umakini, upendo na heshima), kwa hakika wewe hujui ya kwamba huenda hio salaa na salaam zenu zitahudhurishwa mbele yake. Wanafunzi wa Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) waliuliza, “Tufundishe jinsi ya kutuma salaa na Salaam juu ya Rasulullah sallallahu alaihi wasallam ” Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Soma yafuatayo:

اَللّٰهُمَّ اجْعَلْ صَلَوَاتِكَ وَرَحْمَتَكَ وَبَرَكَاتِكَ عَلٰى سَيِّدِ الْمُرْسَلِيْنَ وَإِمَامِ الْمُتَّقِيْنَ وَخَاتَمِ النَّبِيِّيْنَ مُحَمَّدٍ عَبْدِكَ وَرَسُوْلِكَ إِمَامِ الْخَيْرِ وَقَائِدِ الْخَيْرِ وَرَسُوْلِ الرَّحْمَةِ اَللّٰهُمَّ ابْعَثْهُ مَقَامًا مَّحْمُوْدًا يَغْبِطُهُ فِيْهِ الْأَوَّلُوْنَ وَالْآخِرُوْنَ اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدْ اَللّٰهُمَّ بَارِكْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدْ

Ewe Allah ta’ala, Mmiminie baraka na rehema zako makhsusi juu ya kiongozi wa Mitume, Imaam wa waja wote wema, na muhuri wa manabii wote, Muhammad (sallallahu alaihi wasallam), mja wako na mjumbe wako, Imaam wa kheri na wema na mjumbe wa rehema. Ewe Allah ta’ala, mnyanyuwe kwenye nafasi za juu kabisa, na umjaalie kustahiki nafasi ya Maqaam-ul-Mahmood, kwa namna ambayo watu wote kabla yake na baada yake watamuonea wivu. Ewe Allah ta’ala, mmiminie rehema zako Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) na familia ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam), kama ulivyomimina rehema zako juu ya Ibrahim (alayhis salaam) na familia ya Ibrahim (alayhis salaam) Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu zaidi. Ewe Allah (sallallahu alaihi wasallam), mmiminie baraka zako Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) na familia ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam), kama ulivyomimina baraka Zako juu ya Ibrahim (alayhis salaam) na familia ya Ibrahim (alayhis salaam) Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu zaidi.

Wasiwasi wa Mwanamke wa Answaari Kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Katika vita vya Uhud, Waislamu walipata hasara kubwa na idadi kubwa kabisa yao waliuawa. Taarifa nzito zilipofika Madinah Munawwarah, wanawake hao walitoka nje ya nyumba zao wakiwa na shauku ya kutaka kujua undani wa vita hivyo.

Alipouona umati mkubwa wa watu wamekusanyika mahali fulani, mwanamke mmoja waki Answaar aliuliza kwa wasiwasi, “Vipi hali ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)?” Alipoambiwa kuwa baba yake aliuawa vitani, alisema ‘Inna lillahi wa inna ilaihi raaji’uon’ na. kwa kukosa subira alirudia swali lile lile kuhusu Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam).

Wakati huu, aliambiwa kwamba mume wake hayuko tena, kaka yake alikuwa amekufa na kwamba mtoto wake pia aliuawa. Kwa wasiwasi unaozidi kuongezeka, alirudia swali lile lile kuhusu hali ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Aliambiwa kwamba alikuwa salama na mzima, lakini hakutaka kupumzika, na alisisitiza kumwona yeye mwenyewe. Wakati wa mwisho alifurahisha macho yake kwa kumuona yeye mwenyewe na akasema:

كُلُّ مُصِيْبَةٍ بَعْدَكَ جَلَلٌ

“Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), kwa baraka ya kukuona, kila dhiki inapungua na kila wasiwasi huondolewa.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …