CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v62), quality = 90

Sunna na Adabu za Kuchinja – Sehemu ya 3-

11. Ikiwa mtu ana uwezo, ni bora kwake kuchinja mnyama mwenyewe. Ikiwa hili haliwezekani, basi angalau ashuhudie mnyama wake akichinjwa, mradi tu hijaab inazingatiwa kati ya wanaume na wanawake (yaani kuingiliana kusifanyike).

عن علي رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال يا فاطمة قومي فاشهدي أضحيتك فإن لك بأول قطرة تقطر من دمها مغفرة لكل ذنب أما إنه يجاء بلحمها ودمها توضع في ميزانك سبعين ضعفا قال أبو سعيد يا رسول الله هذا لآل محمد خاصة فإنهم أهل لما خصوا به من الخير أو للمسلمين عامة قال لآل محمد خاصة وللمسلمين عامة (الترغيب والترهيب، الرقم: 1662)

Ali (Radhia allaahu ‘anhu) anaripoti kwamba katika tukio moja, Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam) alimwambia Faatimah (radhiallahu ‘anha) “Shuhudia mnyama wako pindi akichinjwa. Kwa tone la kwanza la damu linaloanguka, dhambi zako zitasamehewa. Nyama yake na damu yake vitawekwa katika mizani ya amali zenu na kuzidishwa mara sabini.” Abu Saeed (Radhia allaahu anhu) alimuuliza Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam), “Ewe Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam)! Je, malipo haya yametengwa kwa ajili ya familia yako pekee, kwa vile wanastahiki neema maalum au malipo haya ni kwa Waislamu wote?” Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam) akajibu, “Imeteremshwa makhsusi kuhusiana na familia yangu lakini (fadhila na malipo) pia ni kwa Ummah wangu kwa ujumla.”

12. Mwanamke pia anaweza kuchinja mnyama wake mwenyewe, mradi haonekani mbele ya wanaume.

13. Usimchinje mnyama mbele ya wanyama wengine.

14. Wakati wa kuchinja, mtu atumie kisu kikali na achinje haraka. Mtu asimtie mnyama na maumivu na kumtesa kwa kutumia kisu butu au kumchinja mnyama polepole.

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال أمر رسول الله صلى الله عليه و سلم بحد الشفار وأن توارى عن البهائم. وقال إذا ذبح أحدكم فليجهز (سنن ابن ماجة، الرقم: 3172)

Abdullah bin Umar (Radhia allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam) aliamrisha visu vinolewe (kabla ya kumchinja mnyama), na uchinjaji kufichwe kwa wanyama wengine, na akasema: “Mnapomchinja mnyama, basi mchinje kwa haraka (ili kiasi kidogo cha maumivu impate mnyama).”

15. Usinoe kisu mbele ya mnyama.

عن ابن عباس رضي الله عنهما أن رجلا أضجع شاة وهو يحد شفرته فقال النبي صلى الله عليه وسلم أتريد أن تميتها موتات هلا أحددت شفرتك قبل أن تضجعها (المستدرك على الصحيحين للحاكم، الرقم: 7563)

Ibnu Abbaas (radhiallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba katika tukio moja, mtu alikuwa amemweka mnyama wake chini kwa ajili ya kumchinja na alikuwa akinoa kisu chake (kwa kumtazama mnyama huyo). Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wa sallam) akamkemea akisema, “Je, unataka kumuua mnyama huyu mara nyingi? Kwa nini hukunoa kisu chako kabla ya kuweka mnyama wako chini (ili achinjwe)?”

16. Mtu amlete mnyama mahali pa kuchinja kwa upole. Asimburute mnyama.

عن ابن سيرين قال: رأى عمر بن الخطاب رجلا يسحب شاة برجلها ليذبحها فقال له ويلك قدها إلى الموت قودا جميلا (مصنف عبد الرزاق، الرقم: 8605)

Ibnu Sireen (rahmatullahi ‘alaih) anaripoti kwamba Umar (radhiallahu ‘anhu) aliwahi kumuona mtu akimkokota mbuzi wake kwa mguu wake ili amchinje. Umar (radhiallahu anhu) akamkemea akisema: “Ole wako! iongoze kwenye kifo chake kwa njia nzuri!”

17. Mtu anapaswa kumweka mnyama upande wake wa kushoto kuelekea kibla.

عن أنس قال ضحى رسول الله صلى الله عليه وسلم بكبشين أملحين أقرنين ذبحهما بيده وسمى وكبر ووضع رجله على صفاحهما (صحيح البخاري، الرقم: 5565)

Anas (radhiallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alichinja kondoo dume wawili wenye pembe, mweusi na mweupe. Aliwachinja kwa mkono wake wa baraka huku akisoma tasmiyah na takbira na akaweka mguu wake ubavuni mwao (yaani wanyama walilazwa ubavu wa kushoto ili mnyama aelekee Qiblah).

About admin