Sunna na Adabu za Kuchinja (kwenye siku ya idi kubwa)

1. Kuchinja ni ibaada kubwa na yenye thawabu nyingi katika Dini. Ndani ya Qur-aan Tukufu, kumetajwa kuhusu ibaada ya Kuchinja, na fadhila zake nyingi na umuhimu wake umesisitizwa katika Hadithi ya  Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam). Allah Ta’ala Anasema:

لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ

Si nyama wala damu (ya mnyama) inayomfikia Allah Ta’ala, badala yake ni uchamungu wa moyo wako (ibada ya ukweli) unaomfikia. (Surah Hajj. Aayah 37)

عن زيد بن أرقم رضي الله عنه قال قال أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم : يا رسول الله ما هذه الأضاحي ؟ قال : سنة أبيكم إبراهيم عليه السلام. قالوا : فما لنا فيها يا رسول الله ؟ قال : بكل شعرة حسنة . قالوا : فالصوف يا رسول الله ؟ قال : بكل شعرة من الصوف حسنة (سنن ابن ماجة، الرقم 3127)

Zaid bin Arqam (Radhiya Allaahu anhu) anaripoti kwamba Maswahabah (Radhiallahu anhum) waliwahi kumuuliza Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam ), ni nini umuhimu wa kitendo hiki cha kuchinja? Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) akajibu: “Ni desturi ya babu yako, Ibrahim (‘alaihi salaam).” Kisha maswahaabah wakauliza, “Ewe Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam)! Tutapata thawabu gani kwa kuitekeleza?” Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: “Kwa kila unywele (mgongoni mwa mnyama) utapata ujira.” Kisha Maswahabah wakauliza, “Ewe Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam), vipi kuhusu manyoya? Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) akajibu: “Kwa kila unyoya (mgongoni mwa mnyama) utapata ujira.”

2. Siku ya Idi, kitendo bora na kinachopendwa zaidi na Allah Ta’ala ni kumwagika kwa damu.

عن عائشة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ما عمل آدمي من عمل يوم النحر أحب إلى الله من إهراق الدم، إنه ليأتي يوم القيامة بقرونها وأشعارها وأظلافها، وأن الدم ليقع من الله بمكان قبل أن يقع من الأرض، فطيبوا بها نفسا (سنن الترمذي، الرقم 1493)

Imepokewa kutoka kwa  Aaishah (Radhiya Allaahu anha) kuwa Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) amesema: “Hakuna kitendo chochote anachofanya mmja katika siku za kuchinja ambacho ni kipenzi zaidi na kinachopendwa zaidi na Allaah Ta’ala kuliko kumwagika kwa damu (yaani kumchinja mnyama). Mnyama aliyechinjwa atakuja Siku ya Qiyaamah na pembe zake, nywele zake na kwato zake. Sadaka inakubaliwa na Allah Taala hata kabla damu haijafika ardhini. Kwa hivyo, tekeleza hii ibaada kwa furaha (yaani kwa moyo wako kuwa na furaha na kufurahiya kutekeleza amri ya Allah Taala.)”

3. Kabla ya kuchinja na vilevile wakati wa kuchinja, mtu asimfanyie ukatili mnyama au kumfanyia ubaya kwa namna yoyote ile. Badala yake, mtu anapaswa kumtendea mnyama kwa wema na huruma.

عن شداد بن أوس عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : إن الله تبارك وتعالى كتب الإحسان على كل شيء فإذا قتلتم فأحسنوا القتلة وإذا ذبحتم فأحسنوا الذبح وليحد أحدكم شفرته وليرح ذبيحته.(صحيح مسلم، الرقم 1955)

Shaddaad bin Aus (Radhiya Allaahu ‘anhu) anapokea kwamba Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) amesema: “Allaah Ta’ala Amejaalia wema juu ya kila kiumbe aliye hai. Mnapomuua (adui katika jihaad), basi muueni kwa namna nzuri (yaani msiukate mwili n.k.), na mnapochinja, basi chinjeni kwa njia nzuri na kunowa visu vyenu na kuruhusu mnyama afe kwa urahisi.”

4. Ikiwa mtu ana uwezo, basi ni mustahab kwake kuchinja Kwa njia ya nafl kwa niaba ya Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam), maswahaabah (radhiallahu ‘anhum) na wachamungu wa Ummah.

عن علي رضي الله عنه  أنه كان يضحى بكبشين أحدهما عن النبي صلى الله عليه و سلم والآخر عن نفسه فقيل له فقال أمرني به يعني النبي صلى الله عليه و سلم فلا أدعه أبدا (سنن الترمذي، الرقم 1495)

Imepokewa kuhusu Hadhrat Ali (radhiallahu anhu) kwamba (kila mwaka, wakati wa kuchinja,) alikuwa akichinja kondoo wawili; mmoja kwa niaba ya Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) na mwingine kwa niaba yake mwenyewe. Alipoulizwa (kwa nini alichinja kwa niaba ya Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam)), alijibu: “Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) aliniambia nifanye hivyo, kwa hivyo sitaiacha kitendo hiki kama nipo hai.”

5. Mtu afanye haraka kutekeleza faradhi ya kuchinja. Kutekeleza tendo la kuchinja siku ya kwanza kuna thawabu zaidi kuliko siku ya pili, na kutekeleza siku ya pili kuna thawabu zaidi kuliko siku ya tatu.

عن جابر بن عبد الله قال : شهدت مع النبي صلى الله عليه و سلم الأضحى بالمصلى فلما قضى خطبته نزل عن منبره فأتى بكبش فذبحه رسول الله صلى الله عليه و سلم بيده وقال بسم الله والله أكبر هذا عني وعمن لم يضح من أمتي  (سنن الترمذي، الرقم 1521)

Jaabir (radhiallahu anhu) anaripoti, “Nilikuwepo pamoja na Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) kwenye uwanja wa idi katika siku ya Idi kubwa. Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) alipomaliza khutbah, alishuka kutoka kwenye mimbar (yaani sehemu iliyoinuliwa ambapo alisimama kutoa khutbah) na akaletwa kondoo mbele yake (ya kuchinja). Rasulullah (Sallallahu ‘alahi wasallam) alichinja kondoo kwa mkono wake uliobarikiwa huku akisoma takbeer بسم الله والله اكبر na kusema, ‘hii ni kwa niaba yangu na kwa ajili ya wale waliyo katika Ummah wangu ambao hawanauwezo wa kuchinja (yaani Nafikisha malipo ya kuchinja kwa wale katika Ummah wangu ambao hawawezi kuchinja.’”


 

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 1

1. Unapokutana na ndugu yako Muislamu, muamkie kwa kutoa salaam. Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaripoti …