Sunna na Adabu za Kuchinja – Sehemu ya 2-

6. Ni sunna kwa mtu kujiepusha na kula chochote asubuhi wa Idul Adha (idi kubwa) mpaka arudi kutoka katika swala ya Idi.

عن ابن بريدة عن أبيه رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم كان لا يخرج يوم الفطر حتى يأكل . وكان لا يأكل يوم النحر حتى يرجع (سنن ابن ماجة، الرقم 1756)

Buraidah (radhiallahu anhu) anaripoti kwamba katika siku ya Idul Fitr (idi ndogo), Rasulullah (Sallallaahu ‘alayhi wasallam) alikuwa haondoki (kuswali swala ya idi) mpaka ale kitu chochote. Vile vile, katika siku ya Idul Adha (idi kubwa), hakula chochote mpaka atakaporudi (kutoka kuswali swala ya idi. Aliporudi kutoka kuswali swala ya Idi, kitu cha kwanza alichokula ilikuwa ni ini la mnyama aliyochinjwa).

7. Unaporudi kutoka kwenye Swalah ya Idi, kitu cha kwanza ambacho mtu anatakiwa kula kiwe ni nyama ya mnyama aliyochinjwa (kwa sababu hiki ndicho kilikuwa kitu cha kwanza ambacho Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alikula aliporejea kutoka kwenye Swala ya idi).

حدثني عبد الله بن بريدة، عن أبيه قال: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم لا يغدو يوم الفطر حتى يأكل، ولا يأكل يوم الأضحى حتى يرجع فيأكل من أضحيته (مسند أحمد 38/ 88) وفي رواية البيهقي وكان إذا رجع أكل من كبد أضحيته (السنن الكبرى للبيهقي، الرقم 6161)

Buraidah (radhiallahu anhu) anaripoti kwamba katika siku ya idul Fitr (idi ndogo), Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) alikuwa haondoki kwenda kuswali Idi mpaka ale kitu. Vile vile, katika siku ya Idul Adha (idi kubwa), Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) hakula chochote mpaka aliporudi kutoka kwenye Swala ya idi. Baada ya hapo, kitu (cha kwanza) alichokula kilikuwa ni nyama ya mnyama aliyochinjwa.

Katika riwaya ya Bayhaqi, imepokewa kwamba kitu cha kwanza ambacho Rasulullah (Sallallaahu ‘alayhi wasallam) alikula ilikuwa ini la mnyama uliyochinjwa.

8. Haijuzu kwa mtu kufunga kwenye tarehe 10, 11, 12 na 13 za Dhul Hijjah.

عن نبيشة الهذلي رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم أيام التشريق أيام أكل وشرب وذكر الله (صحيح مسلم، الرقم: 1141، مسند أحمد، الرقم: 20722)

Imepokewa kutoka kwa Nubaisha (Radhiallaahu anhu) kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alayhi wasallam) amesema, “Siku za tashreeq ni siku za kula, kunywa na kumdhukuru Allah Ta’ala.”

9. Mtu ajaribu kwa uwezo wake, kununua mnyama bora kwa ajili ya kuchinja. Jinsi mnyama ana afya zaidi (yaani mwenye thamani zaidi) ndivyo atakavyopata malipo zaidi Akhera.

عن عائشة وعن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه و سلم كان إذا أراد أن يضحي اشترى كبشين عظيمين أقرنين أملحين موجوءين . فذبح أحدهما عن أمته لمن شهد لله بالتوحيد وشهد له بالبلاغ . وذبح الآخر عن محمد وعن آل محمد صلى الله عليه و سلم (ابن ماجة رقم 3122)

Aaishah (radhiallahu anha) na Abu Hurairah (radhiallahu anhu) wameripoti kwamba Rasulullah (Sallallaahu ‘alayhi wa wasallam) alipokusudia kuchinja, alinunua kondoo wawili wakubwa, wenye pembe, mweusi na mweupe, waliohasiwa. Alichinja mmoja kwa niaba ya Ummah wake wote kwa ajili ya wale wanaoshahidilia juu ya tawheedi na juu yake kufikisha (dini kwa Ummah) na mwingine kwa niaba yake na familia ya Nabii (Sallallaahu alayhi wasallam) (yaani: yeye Rasulullah (Sallallahu alayhi wasallam) alifikisha malipo wa mnyama wa kwanza kwa Ummah wake wote, alafu wapili kwa familia yake).

10. Ni mustahab kumnenepesha mnyama kwa ajili ya kumchinja.

قال يحيى بن سعيد سمعت أبا أمامة بن سهل قال كنا نسمن الأضحية بالمدينة وكان المسلمون يسمنون (صحيح البخاري، الرقم 5553)

Yahya bin Sa’eed (rahmatullahi alaih) anaripoti kwamba alimsikia Abu Umaamah bin Sahl (radhiallahu anhu) akisema: “Tulikuwa tukiwanenepesha wanyama wetu wa idi huko Madinah Tayyibah, na Waislamu wote (yaani Maswahaba) walikuwa wakifanya hivyo pia.”

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 1

1. Unapokutana na ndugu yako Muislamu, muamkie kwa kutoa salaam. Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaripoti …