Salaa na Salaam ya Ibrahim (‘alahi salaam)

عن عبد الرحمن بن أبي ليلى قال لقيني كعب بن عجرة فقال ألا أهدي لك هدية سمعتها من النبي صلى الله عليه وسلم فقلت بلى فأهدها لي فقال سألنا رسول الله صلى الله عليه وسلم فقلنا يا رسول الله كيف الصلاة عليكم أهل البيت فإن الله قد علمنا كيف نسلم عليكم قال قولوا اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد (صحيح البخاري، الرقم: 3370)

Abdur Rahmaan bin Abi Laila (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti:

Ka’b bin Ujrah (radhiyallahu ‘anhu) aliwahi kukutana nami na kuniuliza, “Je! nikupe zawadi niliyoipata kutoka kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)? Nilijibu, “Ndiyo, kwa kweli tafadhali nipe hiyo zawadi.” Alisema, “Wakati mmoja, tulimuuliza Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ‘Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), ni Namna gani kukutumia wewe na familia yako salaa na salaam, hakika Allah ta’ala ametufundisha (kupitia kwako) jinsi ya kukutumia salaa na salamu?’” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Sema.

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدٌ اَللّٰهُمَّ بَارِكْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ إِنَّكَ حَمِيْدٌ مَجِيْدٌ

‘Ewe Allah ta’ala, nimiminie rehema zako Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) na familia yake Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) kama ulivyomimina rehema zako juu ya Ibrahim (alahis salaam) na familia ya Ibrahim (alahis salaam) Hakika Wewe ni Mwenye kusifiwa na Mtukufu zaidi. Ewe Allah ta’ala, Mmiminie baraka zako juu ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) familia yake Muhammad (sallallahu alaihi wasallam), kama Ulivyomimina baraka Zako juu ya Ibrahim (alahis salaam) na familia ya Ibrahim (alahis salaam) Hakika Wewe ndiye mwenye kusifiwa na mtukufu zaidi.’

Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) wakiiga Sunnah Mubaraka za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika Kila kitu.

Wakati fulani, mtu mmoja alimwambia Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) , “Allah ta’ala ametaja ndani ya Qur-aan tukufu kuhusu Swalaah kwa amani na Swalaah kwa khofu, lakini hakutaja kuhusu Swalaah wakati wa safari.”

Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) akajibu, “Ewe mpwa wangu! Allah ta’ala alimtuma Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) kama Mtume Wake kwetu tulipokuwa ghaafil na hatujui chochote. Tunapaswa kumfuata katika kila alichofanya.”

Maelezo: Shaikh Moulana Muhammad Zakariyya Kandhelwi (rahimahullah) Kaeleza, “Hii inaonyesha kwamba si lazima kwamba kila sheria ipatikane kwa uwazi katika Quraan Tukufu. Maisha ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na matendo yake ni mwongozo kwetu kufuata. Nabii wa Allah ta’ala amesema, “Nimepewa Quraan Tukufu na pia amri nyinginezo. Jihadharini na wakati unaokuja hivi karibuni wakati watu wasio na wasiwasi wanaketi juu ya vitanda na kusema, ‘Shikamaneni na Qur-aan Tukufu pekee. Tekeleza tu amri zilizomo.’ (Fadaile amaal, Pg, 105)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …