binary comment

Tafseer Ya Surah ‘Aadiyaat.

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلْعٰدِيٰتِ ضَبْحًا ‎﴿١﴾‏ فالْمُوْرِيٰتِ قَدْحًا ‎﴿٢﴾‏ فالْمُغِيرٰتِ صُبْحًا ‎﴿٣﴾‏ فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا ‎﴿٤﴾‏ فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا ‎﴿٥﴾‏ إِنَّ ٱلْإِنسانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ‎﴿٦﴾‏ وَإِنَّهُۥ عَلٰى ذٰلِكَ لَشَهِيدٌ ‎﴿٧﴾‏ وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ‎﴿٨﴾‏ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ ‎﴿٩﴾‏ وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ ‎﴿١٠﴾‏ إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرُ ‎﴿١١﴾

(Naapa) kwa wale (farasi) waendao mbio kwa kuhema kwa pumzi, Na wakitengeneza cheche kwa kuzipiga (kwato zao) kwenye ardhi ya mawe (wanapokimbia), Na wakishambulia alfajiri, Na wakitimua vumbi nalo, Na wakijituma kati ya maadui. Hakika mwanadamu ni mwenye kumkufuru sana Mola wake. Na yeye ni shahidi wa ukweli huu. Na katika upendo wake wa mali, yeye ni mkali sana. Je, basi hajui (yatakayotokea) yatakapopinduliwa vilivyomo makaburini? Na yote yaliyomo ndani ya vifua (nyoyo) yatadhihirika. Hakika Mola wako siku hiyo atakuwa na habari zao zote.

Katika surah hii, mwanadamu ameitwa kutafakari juu ya asili ya farasi na kiwango chake cha utii na uaminifu kwa mmiliki wake. Farasi ni mnyama ambaye anayeitikia kwa utii amri ya mwanadamu. Yupo tayari kutoa dhabihu ya aina yoyote kwa ajili ya mmiliki wake, hata kama itahitajika kuutoa uhai wake katika makali ya vita. Wakati wowote wa usiku au mchana, ikiwa mwanadamu atamwita mnyama huyu, atajibu kwa urahisi bila kusita. Anapoipanda na kwenda vitani, itajituma ndani kabisa ya maadui, ikihatarisha uhai wake kwa ajili yake. Silaha za adui hazitaizuia kwa njia yoyote ile kutimiza amri ya mmiliki wake.

Hiki ndicho kiwango cha uaminifu na shukrani ambacho farasi huonyesha kwa mmiliki wake, ingawa upendeleo wa mmiliki was farasi ni mdogo kwa kulinganisha na upendeleo was farasi. Yote ambayo mwanadamu humfanyia ni kumpa chakula cha mifugo na kuionyesha kujali kwa kiwango kidogo, lakini farasi huyo anathamini sana kwamba atamlipa kwa kutoa uhai wake kwa ajili yake.

Hivyo basi, ujumbe ambao Allah Ta’ala anatupa kupitia Aya hizi ni, Ewe mwanadamu! Tazama ndani yako na uone jinsi unavyomshukuru Mola wako. Je, unaonyesha shukrani na uthamini sawa na uthamini ambao mnyama huyu asiye na akili huonyesha kwa mmiliki wake? Ikiwa mnyama huyu ambaye hana ufahamu na akili ya mwanadamu anaweza kuonyesha kiwango cha juu cha shukurani na uaminifu, basi ni kiwango gani cha shukurani na uaminifu kinachotarajiwa kwako kumuonyesha Allah Ta’ala, ukizingatia kwamba Allah Ta’ala amekubariki kwa ufahamu na maarifa na kila aina ya fadhila?

إِنَّ ٱلْإِنسانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ‎﴿٦﴾

Hakika mwanadamu ni mwenye kumkufuru sana Mola wake.

Aya hii imetanguliwa na kiapo kinachochukuliwa juu ya sifa tofauti za farasi wanaotumiwa katika vita. Jambo linalozungumziwa ni kwamba ingawa Allah Ta’ala amemfanya mnyama huu mwenye nguvu kiasi kuwa chini ya amri ya mwanadamu, badala ya mwanadamu kuthamini fadhila hii ya Allah Ta’ala, na kuwa mtiifu kwa Allah Taala kama vile farasi ni mtiifu kwake, yeye mwanadamu anabaki kuwa hana shukurani kwa Allah Taala.

Kwa hiyo, katika Aya hii, Allah Ta’ala anamlalamikia mwanadamu kuwa yeye anamkufuru sana Mola wake. Neno ‘kanood’ ambalo Allah Ta‘ala alitumia kumuelezea mwanadamu, linamrejelea mtu ambaye anakumbuka shida na matatizo yanayompata, lakini akasahau neema na fadhila anazozifurahia. Hii ndiyo asili ya mwanadamu- anafurahia fadhila za Muumba wake, lakini anamsahau yule Aliyempa neema hizi. Anazama katika kufurahia neema za Allah Ta’ala kiasi kwamba anasahau kwamba kila alichopata ni kwa rehema na fadhila za Allah Ta‘ala ambae ni Mwingi wa kurehemu na Mwenye kufadhili. Anapoteza uwezo wa kuona na kusahau kwamba fadhila hizi zote na neema hazipatikani kwa sababu ya akili yake mwenyewe.

وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ‎﴿٨﴾

Na katika upendo wake wa mali, yeye ni mkali sana.

Katika aya hii, Allah Ta’ala analaani sifa wa kuwa na mapenzi makubwa ya mali. Mapenzi ya mali si haraam, lakini kupenda mali kupita kiasi haijuzu kwa sababu humfanya mtu kusahau faradhi zake anazowiwa na Muumba wake pamoja na waja wa Allah Ta‘ala. Kuna wakati fulani, kwa sababu ya kupenda mali kupita kiasi, mtu hatatofautisha kati ya halali na haraam, au hatajishughulisha na kutekeleza matendo ambayo yatamchukiza Allah Ta’ala.

Hivyo basi, chanzo kikuu cha matatizo yote ni kupenda mali kupita kiasi. Kwa hiyo, Allah Ta’ala anaagiza dawa ya kutibu mojawapo ya mapenzi na shauku kubwa ya mali. Dawa ni kwamba mwanadamu anatakiwa kutafakari na kukumbuka mara kwa mara mwisho wake pamoja na Siku ya Qiyaamah, atakaposimama mbele ya Allah Ta‘ala.

أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ ‎﴿٩﴾‏ وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ ‎﴿١٠﴾‏ إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرُ ‎﴿١١﴾

Je, basi hajui (yatakayotokea) yatakapopinduliwa vilivyomo makaburini? Na yote yaliyomo ndani ya vifua (nyoyo) yatadhihirika. Hakika Mola wako siku hiyo atakuwa na habari zao zote.

Katika aya hiyo hapo juu, Allah Ta‘ala anavuta mazingatio yetu kuelekea katika Siku ya Qiyaamah. Siku hiyo kila kinachofichika kitafichuliwa mbele ya wote. Yaliyomo makaburini yatapinduliwa, na yaliyofichika nyoyoni yatadhihirika. Nia zote zilizofichwa na mwanadamu moyoni mwake zitadhihirika Siku ya Hukumu. Ikiwa mtu alifanya kitendo cha wema na kitendo cha kujionyesha, basi siku hiyo nia yake potovu itafichuliwa na kufichuliwa mbele ya watu wote.

About admin

Check Also

Tafseer Ya Surah Lahab

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ‎﴿١﴾‏ مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ‎﴿٢﴾‏ سَيَصْلَىٰ نَارًا …