عن ابن عباس أنه كان يقول: اللهم تقبل شفاعة محمد الكبرى وارفع درجته العليا وآته سؤله في الآخرة والأولى كما آتيت إبراهيم وموسى (مصنف عبد الرزاق، الرقم: 3104، وإسناده جيد قوي صحيح كما في القول البديع صـ 122)
Ibn Abbas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba alipokuwa akimtumia salaa na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akiisoma kwa maneno yafuatayo:
اَللّٰهُمَّ تَقَبَّلْ شَفَاعَةَ مُحَمَّدٍ الْكُبْرٰى وَارْفَعْ دَرَجَتَهُ الْعُلْيَا وَآتِهِ سُؤْلَهُ فِيْ الْآخِرَةِ وَالْأُوْلٰى كَمَا آتَيْتَ إِبْرَاهِيْمَ وَمُوْسٰى
Ewe Allah, ukubali uombezi wa Muhammad (sallallahu alaihi wasallam)(yaani uombezi wakati ambapo mataifa yote yatakuwa katika matatizo mahali ya kufufuliwa) na umnyanyue daraja la juu, na mpe anachokitaka katika Aakhirah na dunia hii kama ulivyowapa Nabi Ibrahim na Nabi Musa (alayhi mus salaam).
Abdullah bin Amr (radhiyallahu ‘anhuma) Anachoma Nguo Yake.
Abdullah bin Amr bin Al-Aas (radhiyallahu ‘anhuma) anasema:
Wakati fulani tulikuwa tukifuatana na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika safari. Nilienda kumuona na nilikuwa nimevaa shuka la rangi ya zafarani. Yeye akaniuliza, “Ni nini hiki ulichokivaa?” Nilihisi kwamba akupenda rangi cha kitamba nilichovaa. Kwa hiyo, nilipofika nyumbani na kukuta moto ukiwaka, nilitupa vazi langu ndani ya moto.
Siku iliyofuata, nilipoenda kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akauliza, “ile nguo ipo wapi?” nilipomjulisha nilichokifanya nacho, alisema, “Ungeweza kumpa mmoja wa wanawake wa nyumbani kwako. Wanawake wanaruhusiwa kuvaa nguo za rangi hiyo.”
Abdullah bin Amr bin Al-Aas (radhiyallahu ‘anhuma) alifadhaika sana na kukasirika kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwamba hakusita kutumia fursa ya kwanza ya kuliondoa lile nguo lililosababisha hasira. Hakufikiria hata kutafuta matumizi mengine ya vazi hilo. Kama tungelikuwa katika nafasi yake, tungelifikiria udhuru tofauti wa kuiweka, au angalau kutafuta matumizi mengine.