Salaa na Salaam Maalum juu ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: من قال اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وآل إبراهيم وبارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وآل إبراهيم وترحم على محمد وعلى آل محمد كما ترحمت على إبراهيم وآل إبراهيم شهدت له يوم القيامة بالشهادة وشفعت له (الأدب المفرد، الرقم: 641، وهو حديث حسن ورجاله رجال الصحيح لكن فيهم سعيد بن عبد الرحمن مولى ال سعيد بن العاص الراوي له عن حنظلة، وهو مجهول لا نعرف فيه جرحا ولا تعديلا، نعم ذكره ابن حبان على قاعدته كما في القول البديع صـ 112)

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Yoyote atakayesoma yafuatayo (salaa na salaam), nitatoa ushahidi kwa niaba yake siku ya Qiyaamah na nitamfanyia uombezi.”

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ وَبَارِكْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ وَتَرَحَّمْ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَعَلٰى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا تَرَحَّمْتَ عَلٰى إِبْرَاهِيْمَ وَعَلٰى آلِ إِبْرَاهِيْمَ

Ewe Allah subhaana wata’ala! Tuma salaam kwa Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) na Familia ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) kama ulivyomtumia Ibrahim (alayhis salaam) salaam na familia ya Ibrahim (alayhis salaam) na baraka zimshukie Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) na familia ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) kama ulivyommiminia Ibrahim (alayhis salaam) na familia ya Ibrahim (alayhis salaam) na baraka. Rehema zimashukie Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam) na familia ya Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam), kama ulivyommiminia rehema Ibrahim (alayhis salaam) na familia ya Ibrahim (alayhis salaam).

Ansaari anabomoa jengo mpaka chini.

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikuwa akipitia barabara ya Madinah Munawwarah alipoona jengo likubwa. Akauliza kutoka kwa Swahaabah, “Ni nini hiki?” Wakamjulisha kwamba lilikuwa ni jengo jipya lililojengwa na Ansaari mmoja. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akakaa kimya.

Wakati mwingine, Ansaari yule aliyojenga nyumba hiyo alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kumsalimia kwa salamu. Basi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) aligeuza uso wake, mbali yeye alirudia tena lakini hakujibu. Sahaabi huyu alikuwa na wasiwasi sana kwa ajili ya Rasulullah akujibu salaam yake.

Alipouliza kutoka kwa Maswahabah, walimfahamisha kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alipita karibu na jengo lipya alilokuwa amelijenga na kuiulizia. Hapo hapo akaenda na kulibomoa hilo jengo lipya chini, na hata hakumjulisha Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuhusu kitendo chake.

Muda fulani baadaye, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alitokea kupita njia hiyo tena. Aliuliza, “Liko wapi lile jengo kubwa ambalo nakumbuka kuliona mara ya mwisho tulipopita hapa?” maswahaabah walimjulisha kama yule answaari alilibomoa mpaka chini, kwa vile alihisi kuwa hiyo ndiyo sababu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuchukizwa. Wakati huo, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Alisema, “Kila muundo (ambao umejengwa bila hitaji la kweli) utakuwa mzigo kwa mtu, isipokuwa ule muundo ambao ni muhimu sana.”

Kitendo cha huyu Sahaabi ulionyesha upendo wa kweli na kujitolea. Na Maswahaabah hawakuweza kuvumilia kukasirika kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), na mara tu walipohisi kuchukizwa kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kupitia kitendo chochote kile, mara moja waliacha kitendo hicho kwa gharama yoyote ile. (Sunan Abi Dawood, #5237)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …