Abu sa'eed khudri (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, muislamu yoyote ambaye hana chochote kutoa kama sadaqa, inabidi amtumie Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) hii salaam kwenye dua yake kwa sababu ni njia ya yeye kupata thawabu ya sadaqa na itamsafishia madhambi zake."
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl – Sehemu Ya Pili
4. Kama unafanya ghusl ndani ya shawa basi hakikisha autumii maji vibaya. Usijishughulishe na kupaka sabuni au kunyowa nywele zisizohitajika (mf: makwapani na sehemu za siri) wakati bomba la maji lipo wazi. Huu ni uharibifu mkubwa na nisababu ya kupata madhambi
Soma Zaidi »Kupokea Cheti cha Uhuru kutokana na Unafiki na moto wa Jahannam
Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, "yoyote atakae nitumia salaam mara moja, kwa kumlipa Allah subhaana wata'alah atamtumia salamu mara kumi (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara kumi, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam mara mia (yaani: ataampa zawadi na atamfariji na rehma zake), na yoyote atakae nitumia salaam mara mia, Allah subhaana wata'alah Atamwandikia (cheti) uhuru, katikati ya macho yake mawili, kutokana na unafiki, (na cheti ya) uhuru kutokana na moto wa jahannum, na Allah subhaana wata'alah ataampa heshma na faraja ya kuwa na mashahidi siku ya qiyamah."
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Ghusl – Sehemu Ya Kwanza
1. Elekea qibla ukiwa unafanya ghusl. Ni vizuri kuvaa nguo kufunika sehemu za siri ukiwa unaoga.
2. Oga kwenye sehemu ambayo mtu hawezi kukuona. Ni vizuri kuoga na sehemu za siri zikiwa zimefunikwa. Hata hivyo inaruhusiwa kama mtu yuko sehemu iliyofungwa (mf: bafuni) na mtu anaoga bila kufunika sehemu za siri.
Soma Zaidi »Njia Za Sunna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Nane
24. Usitumie maji vibaya ukiwa unafanya udhu.
Sayyidina Abdullah Bin Amr (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alipita kwa Sayyidina Sa'd (radhiyallahu anhu) akiwa anafanya udhu. Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimuuliza, "huu uharibifu ni wanini (ya maji kwenye udhu wako)?" Alijibu, "kwani kuna uharibifu kwenye udhu?" Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) alimjibu, "ndiyo hata kama unafanya udhu ukingoni mwa mto (pia, kuwa makini kutoharibu maji).
Soma Zaidi »Mtu Kuona Makazi Yake Peponi
Sayyidina Anas (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) amesema, "anaye soma salaamu kwangu mara elfu moja kwa siku ya ijumaa hata kufa mpaka aonyeshwe nafasi yake katika peponi."
Soma Zaidi »Njia Za Sanna Za Kufanya Udhu -Sehemu Ya saba
20. Osha viungo vya upande wa kulia kabla viungo vya upande wa kushoto.[1] عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا لبستم وإذا توضأتم فابدءوا بأيامنكم (سنن أبي داود، الرقم: ٤١٤١)[2] Sayyiduna Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Sayyiduna Rasulullah (sallallahu alaih wasallam) …
Soma Zaidi »Kufanya musaafaha na Nabii wa Allah (sallallahu alaih wasallam) kwa siku ya mwisho
Imeripotiwa kwamba Nabii (sallallahu alaih wasallam) amesema "yoyote atakaye niswalia mara khamsini kila siku, nitafanya musaafaha (kushikana mikono) na yeye siku ya mwisho."
Soma Zaidi »Njia Za Sanna Za Kufanya Udhu -Sehemu Ya Sita
Baada ya kumaliza kufanya udhu, soma shahada. Kama uko sehemu iliyo wazi, angalia mbiguni ukiwa unasoma shahada.[1] Vile vile soma dua zingine ambazo zimetajwa katika hadith.
Soma Zaidi »Mahitaji yote ya dunia na ya deeni kutimizw
Habbaan Bin Munqiz (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba sahabi moja aliwahi kumuuliza Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam), "Ewe mjumbe wa Allah (sallallahu alaih wasallam) je nijitolee thuluthi moja ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alijibu, "ndio, kama utapenda." Ule sahabah akauliza, "je nijitolee thuluthi mbili ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah akajibu tena, "ndio, kama utapenda. "ule sahabah akauliza, "je nijitolee muda wote kukutumia salaam? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) akajibu, "kama utafanya hivyo, Allah subhaana wata'alah Atayatimiza mahitaji yako yote ambayo unayo (na amboyo ungeulizia kwenye dua yako), ikiwa niyakuhusu dunia au aakhera."
Soma Zaidi »