Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا مجالسكم بالصلاة علي فإن صلاتكم علي نور لكم يوم القيامة (الفردوس بمأثور الخطاب، الرقم: ٣٣٣٠، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٨)

Ibnu umar (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alisema, “Pamba mikusanyiko yenu na kunitumia salaam, kwa sababu siku ya qiyaama, salamu zenu juu yangu itakuwa nuru (sababu ya nuru) kwenu.”

Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) akiwa Tayari kutoa Kila Kitu kwa ajili ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Wakati wa vita vya Badr, mtoto wa Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu), Abdur Rahmaan (radhiyallahu ‘anhu), alipigana upande wa makafiri kwa vile alikuwa bado hajaukubali Uislamu.

Baadaye, baada ya kusilimu, akiwa amekaa na baba yake, Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) akasema, “Ewe baba yangu kipenzi! wakati wa vita vya Badr, ulikuja chini ya upanga wangu mara chache. Hata hivyo, kwa kuzingatia wewe kuwa baba yangu, nilikuacha.”

Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) akajibu mara moja, “Ingekuwa wewe kuingia chini ya upanga wangu wakati wa vita, nisingeweza kamwe kukuacha, kwa sababu mlikuwa mnapigana kumpinga Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam). (Tareek Ul Kulfaa, 1/33)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …