Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) baada ya kusikia adhaan

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول إذا سمعتم المؤذن فقولوا مثل ما يقول ثم صلوا علي فإنه من صلى علي صلاة صلى الله عليه بها عشرا ثم سلوا الله لي الوسيلة فإنها منزلة في الجنة لا تنبغي إلا لعبد من عباد الله وأرجو أن أكون أنا هو فمن سأل لي الوسيلة حلت له الشفاعة (صحيح مسلم، الرقم: 384)

Abdullah bin Amr bin Al-Aas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba alimsikia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akisema, “Unapomsikia Muadhin akitoa adhaan, basi rudia maneno ya adhaan baada yake na baada ya hapo nitumie salaa na salaam (kabla ya kusoma dua ya adhaan). Hakika, mwenye kunitumia salaa na salaam mara moja, Allah subhaana wata’ala humteremshia baraka kumi juu yake. Kisha (soma dua baada ya adhaan ambayo ndani yake) unaomuomba Allah subhaana wata’ala Anijaalie utukufu wa ‘waseelah’ ambao ni nafasi na daraja ya juu katika Jannah ambayo itatolewa kwa mja wa kipee wa Allah subhaana wata’ala Natumaini kwa dhati kwamba nimepewa hiyo nafasi, na yoyote anayeomba kwa Allah subhaana wata’ala kwamba anijaalie ‘waseelah’, atapata uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”

Mapenzi ya maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Mtu fulani aliwahi kumuuliza Ali (radhiyallahu ‘anhu), “Ni mapenzi ya dhaati ya kiasigani maswahaabah walikua nayo kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ?”

Ali (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Mimi na aapa kwa Allah subhaana wata’ala, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa kipenzi zaidi kwetu kuliko mali yetu, watoto wetu na mama zetu, na kuwa karibu nae ilikuwa ni bora zaidi kuliko kinywaji cha maji baridi wakati wa kiu kali.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …