Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) baada ya Kusikia Adhaan

عن جابر رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من قال حين يسمع النداء اللهم رب هذه الدعوة التامة والصلاة  القائمة آت محمدا الوسيلة والفضيلة وابعثه مقاما محمودا الذي وعدته حلت له شفاعتي يوم القيامة (صحيح البخاري، الرقم: 614 ،وأما زيادة إنك لا تخلف الميعاد فقد ذكرها البيهقي في السنن الكبرى، الرقم:١٩٩٤ ،وقال عنها السخاوي في المقاصد الحسنة صـ 343 :وهو عند البيهقي في سننه فزاد في آخره مما ثبت عند الكشمهين في البخاري نفسه إنك لا تخلف الميعاد)

Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu  alaihi wasallam) alisema, “Mwenye kusoma dua ifuatayo baada ya Adhaan, atapata uombezi wangu siku ya Qiyaamah.”

اللهم رب هذه الدعوة التامة والصلاة  القائمة آت محمدا الوسيلة والفضيلة وابعثه مقاما محمودا الذي وعدته إنك لا تخلف الميعاد

Ewe Allah subhaana wata’ala, Mola wa wito huu mkamilifu na wa Swalaah uliyoweka, mjaalie Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) Waseelah (sehemu ya juu sana katika Jannah) na ‘fadheelah’ (nafasi ya juu iliyo juu ya viumbe vyote), na mpe “Maqaam-ul- Mahmood” (yaani heshima ya kuombea uombezi kwa Allah subhaana wata’ala aanze hisaab ya viumbe vyote siku ya Qiyaamah) uliyomuahidi. Hakika huendi kinyume na ahadi yako.

Mapenzi ya Zaid bin Dathinah (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Makafiri walipokaribia kumuuwa sahabi mkubwa, Zaid bin Dathinah (radhiyallahu ‘anhu), wakamuuliza, “Je, ungekuwa na furaha zaidi kama Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) angekuwa katika nafasi yako na ukaachwa huru kuwa pamoja na familia yako?”

Jibu lake la papo kwa papo lilikuwa, “Wallahi, siwezi hata kustahimili kuwa nimekaa kwa raha na familia yangu huku hata mwiba unamchoma Rasulullah (sallallahu  alaihi  wasallam)  aliposikia haya, Abu Sufyaan alisema, “Hakuna mfanano popote duniani na upendo ambao maswahaba wa Muhammad (sallallahu  alaihi  wasallam) wanao kwake.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …