Dua nyingine itakayosomwa baada ya Adhaan

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : ما من مسلم يقول إذا سمع النداء فيكبر المنادي فيكبر ثم يشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله فيشهد على ذلك ثم يقول اللهم أعط محمدا الوسيلة واجعل في عليين درجته وفي المصطفين محبته وفي المقربين داره الا وجبت له شفاعة النبي صلى الله عليه و سلم يوم القيامة (شرح معاني الاثار، الرقم: ٨٩٤)

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)  kasema: “Muislamu yoyote atakaye sikia Adhaan ikitolewa, na kujibu takbira ya muadhin kwa kusoma takbira, na kujibu shahaadah ya muadhin kwa kusoma shahaadah, na baada ya hapo anasoma dua ifuatayo, atapata uombezi wa Nabii wa Allah (sallallahu  alaihi  wasallam)  Siku ya Qiyaamah:

اللهم أعط محمدا الوسيلة واجعل في عليين درجتهوفي المصطفين محبته وفي المقربين داره

Ewe Allah subhaana wata’ala, mbariki Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) kwa Waseelah ya kuombea viumbe vyote siku ya Qiyaamah, na Inyanyuwe hatua yake mpaka daraja ya juu kabisa katika iliyooni (Peponi), na ubariki mioyo ya watumishi wako uliowachagua kwa upendo wake, na uwabariki wachamungu miongoni mwa  waja wako pamoja na marafiki wake katika Akhera.

Mapenzi ya Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Katika tukiyo la Hudaybiyah, Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameamrishwa na Rasulullah (sallallahu  alaihi wasallam)  kujadiliana na Maquraishi huko Makka Mukarramah. Wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameondoka kwenda Makka Mukarramah, baadhi ya Maswahaba walimwonea wivu Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa kuweza kufanya tawaaf ya Nyumba ya Allah subhaana wata’ala Kwa upande mwingine, Rasulullah (sallallahu  alaihi  wasallam) alisema, “Sidhani kama atatamani kufanya tawaaf bila mimi.”
Wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alipoingia Makkah Mukarramah, Abaan bin Said (radhiyallahu ‘anhu) akamchukua kwenye hifadhi yake na akamwambia:

“Unaweza kuzunguka kwa uhuru popote unapotaka. Hakuna mtu hapa anaweza kukugusa.”

Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alifanyamazungumzo yake na Abu Sufyaan na wengine wa Makkah Mukarramah kwa niaba ya Nabii wa Allah sallallahu alaihi wasallam na alipokuwa karibu kurejea,

Waquraishi wenyewe walimwambia, “Sasa ukiwa humu ndani Makkah Mukarramah, unaweza kufanya tawaaf kabla ya kurudi.”

Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Itawezekana vipi nifanye tawaaf (bila ya Nabii Muhammad sallallahu alaihi wasallam)?”

Jibu hili haikuwafurahisha Maquraish na wakaamua kumzuwiya  Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ndani ya Makkah Mukarramah. Habari imewafikia Waislamu kama Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) amefariki kishahidi. Pindi habari hii ilimfikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), alikula kiapo cha utii kutoka kwa Maswahabah wote kupigana mpaka tone la mwisho la damu yao. Maquraishi walipo fahamu haya, hofu iliwaingia na mara moja wakamwachilia Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …