وعن سهل بن عبد الله قال من قال في يوم الجمعة بعد العصر اللهم صل على محمد النبي الأمي وعلى إله وسلم ثمانين مرة غفرت له ذنوب ثمانين عاماً أخرجه ابن بشكوال وقد تقدم قريباً في حديث أبي هريرة معناه (القول البديع صـ 400)
Imepokelewa na Sahl bin Abdullah (radhiyallahu ‘anhu), “Yoyote atakaye tuma salaa na salaam ifuatayo mara thamanini baada ya al-asiri siku ya Ijumaa, dhambi zake za miaka thamanini zitasamehewa.
اللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ وَعَلٰى آلِهِ وَسَلِّمْ
Ewe Allah, tuma salaa na salaam tele juu ya Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam), Nabi asiye jua kusoma, na juu ya familia yake.
Sayyidina Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) ndani ya pango la Thaur
Wakiwa ndani ya pango katika safari ya hijrah, imepokelewa kuwa Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa na wasiwasi kwamba asitokee mdudu yeyote kwenye shimo lolote ndani ya pango na kumdhuru Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kwa hivyo, alianza kufunika shimo zote ndani ya pango kwa kutumia vipande vya nguo yake ya chini. Hata hivyo, bado kulikuwa na Mashimo mawili ambayo hakuweza kuyafunika (kutokana na nguo kutotosheleza), basi Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) akaweka miguu yake yote miwili kwenye mashimo hayo. Baada ya hapo, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akaweka kichwa chake cha baraka kwenye mapaja ya Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) na akalala.
Wakati Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akiwa amelala, Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) aligundua kuumwa na nyoka chini ya mguu wake kutoka kwenye shimo. Kutokutaka kusumbua usingizi wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa uchache zaidi, Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) alivumilia maumivu na hakusonga hata hatua moja. Lakini, kuwa na maumivu makali na kutoweza kuvumila athari, machozi yalianza kutoka bila kujizuia kwenye uso wa Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) na yakaanguka kwenye uso wa mubaarak wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)
Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akaamka na kuuliza: “Ni nini kimetokea ewe Abu Bakr?” Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Nimeumwa na nyoka, wazazi wangu watolewe kafara kwa ajili yako Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) aliweka mate yake ya mubaarak kwenye eneo liliyoathiriwa, na maumivu yakapungua mara moja. (Miskaat, #6034)