Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) ukiwa kwenye Mkusanyiko.

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا مجالسكم بالصلاة علي فإن صلاتكم علي نور لكم يوم القيامة (الفردوس بمأثور الخطاب، الرقم: ٣٣٣٠، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ 278)

Abdullah Bin Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “pendezesheni mikusanyiko yenu kwa kuniswalia. Kwa sababu swalaa na salaam zenu juu yangu itakuwa nuru kwenu Siku ya Qiyaamah.”

Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) Akimpa Maziwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) anaeleza kuhusu safari ya Hijrah pamoja na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Tulisafiri kwa haraka mchana na usiku mzima hadi joto la jioni likawa kali. Kisha nikakuta barabara kuwa tupu na hakuna mtu hata mmoja alikuwa akitembea kwenye barabara, nilitazama mbele kuona kama ningeweza kupata kivuli chochote ili tuweze kujificha humo. Kisha nikaona pango ambamo tungeweza kukimbilia na kutafuta hifadhi kutokana na joto. Kisha nikasema, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), baki kwanza nje ya pango na niruhusu niingie ili kama kuna kiumbe chenye madhara ndani ya pango, itanidhuru mimi na si wewe.”

Baada ya kuingia ndani ya pango hilo nilianza kulisafisha na kutandaza kitambaa ambacho Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) angeweza kulalia. Kisha nikaomba aingie na kupumzika na akakubali ombi langu. Pindi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alijilaza kupumzika, nilikwenda kuangalia kama nitaweza kumwona mtu yoyote aliyekuwa akitutafuta. Kisha nikamwona mchungaji fulani aliyekuwa mtumwa karibu na kumuuliza ni nani mmiliki wake.

Akamtaja mtu mmoja kutoka Makka ambaye nilimfahamu. (Kama ilivyokuwa desturi wakati huo kwamba watu kuruhusu wasafiri kunufaika na maziwa kutoka kwa mifugo yao, Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) aliomba maziwa na mazungumzo yafuatayo yaliongelewa):

Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) : “Je kuna mbuzi yoyote ana maziwa?”

Mchungaji: “Ndiyo.”

Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu): “Je, utanikamulia?”

Alikubali, na kunikamulia maziwa ya mbuzi mmoja na kuyamimina ndani chombo changu. Niliongeza maji kwenye maziwa ili kupoza maziwa ya moto. Kisha nikachukua maziwa kumkabidhi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Wakati nilimsogelea Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), nilimkuta macho. Nikasema, “Kunywa haya maziwa, Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam ”.Kumuona Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kufurahiya maziwa kulileta furaha nyingi kwa moyo wangu.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …