Monthly Archives: March 2021

Kupata Rehma Kumi

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu 'anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema " yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata'alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi" 

Soma Zaidi »

Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaanahu Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu 'alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa.

Soma Zaidi »

Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili

4. Osha mikono yote mpaka kwenye vifundo mara tatu

Sayyidina Humraan (rahimahullah), mtumwa aliye huru wa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu)aliomba aletewe maji (kuonyesha watu jinsi gani ya kuchukuwa udhu). Kisha alianza kutawadha kwa kuosha mikono (mpaka kwenye vifundo) mara tatu. (kwenye riwaya hii, iliyopatikana ndani ya Sahihi Bukhari, Sayyidina Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kasema ” nilimuona Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) anafanya udhu kwa namna hii.)”

Soma Zaidi »

Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Tano

17. Chukuwa tahadhari sana kuhakikisha kuwa hupatwi na cheche za mkojo mwilini. Hukifanya uzembe kwa hili kuna adhabu kaburini.

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) alisema kuwa mtume (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” adhabu kali (zitakazo wakabili watu wengi) kaburini ni adhabu za mkojo (mf: mtu kutokuwa makini kwa cheche za mkojo ambazo zinampata. Kwa ajili ya hilo udhu, sala zao na ibada zingine hazitokubalika kwa kuwa mtu anakuwa mchafu”)

Soma Zaidi »

Aina Za Sunna Za Kufanya Istinja – Saheemu Ya Nne

11. Usizungumze ukiwa unajisaidia, labda kuwe na shida muhimu wa kuongea.

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu 'anhu) alitowa taarifa kuwa Nabii wa Allah subhaana wata'alah (sallallahu 'alaihi wassallam) amesema "watu wawili wasiende pamoja kujisaidia sehemu moja na kuongea pamoja wakiwa watupu (yaani sehemu zao za siri) ziko wazi kwa hakika mwenyezi mungu hapendi kitendo hicho.

Soma Zaidi »