Kupata Rehma Kubwa Za Allah Subhaana Wata’alah

عن ابن عمر وأبي هريرة رضي الله عنهما قالا قال رسول الله صلى الله عليه وسلم صلوا علي صلى الله عليكم (الكامل لابن عدي، الرقم: ١١٠٨٦، وإسناده ضعيف كما في التيسير للمناوي ٢/٩٣)

Sayyidina Abdullah Bin Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) wamesema kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “Nitumieni salaam kwangu, Allah subhaana wata’alah atawafariji na rehma”

Ukombozi Kupitia Kumsalia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Mara Nyingi

Siku moja mtu alimuona sheikh Abu Hafs Al kaaghazi (rahimahullah) ambae alikuwa mchamungu sana, katika ndoto baada ya kufa kwake. Baada ya kumuona sheikh Abu Hafs (rahimahullah) alimuuliza, “Allah subhaana wata’alah amedili na wewe vipi?” Sheikh Abu Hafs (rahimahullah) alijibu, “Allah subhaana wata’alah alikuwa na rehma juu yangu, amenisamehe na ameniingiza peponi”. Pindi Sheikh Abu Hafs alivyo ulizwa sababu ya kuheshimiwa na kupata baraka kwa njia hii, alisema, ” pindi niliposimama mbele ya Allah subhaana wata’alah, Allah Ta’ala aliwamrisha malaika kuanza kuhesabu matendo yangu. Walianza kuhesabu madhambi yangu na walihesabu salaam zangu za kumsalia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wassallam) na wakakuta salaam zangu kwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ni zaidi kuzidi madhambi yangu. Kisha Allah subhaana wata’alah aliwambia malaika, enyi malaika wangu hii inatosha! Usimchukuwe kwa hesabu ya madhambi zake, badala muingizeni kwenye pepo yangu.”” (Al-Qowlul Badee’ Pg. 259)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …