Kupata Rehma Kumi

عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: من صلى علي واحدة صلى الله عليه عشرا (صحيح مسلم،  الرقم: ٤٠٨)

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata’alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi” 

Kumsaliya Nabii (Sallallahu ‘Alaihi Wassallam) Mara Elfu Moja Kila Siku

Sheikh Abul Hasan Baghdaadi Ad-daarimi (rahimahullah) amesema:  Nimemuona mara nyingi Abu Abdullah Haamid (rahimahullah) kwenye ndoto baada ya kifo chake. Nilimuuliza kitu gani ambacho kimempata  hakasema, allah subhaana wata’alah amenisamehe na amenihurumia’ kisha nikamuuliza nakuomba niambie kitendo kimoja, ambacho kitaniingiza moja kwa moja peponi.” Alijibu, ” swali nafli rakaat elfu moja, na kwenye kila rakaat soma sura ikhilaas mara elfu moja” nikamjibu ” lakini kwa hakika hili ni tendo gumu sana kulifanya.” Hakasema, kwahiyo,  msalie Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) Mara elfu moja kila usiku” Abul Hasan alisema zaidi, huu ulikuwa utaratibu wangu tangu wakati ule.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …