Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaanahu Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن عبد الرحمن بن عوف رضي الله عنه قال خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فاتبعته حتى دخل نخلا فسجد فأطال السجود حتى خفت أو خشيت أن يكون الله قد توفاه أو قبضه قال فجئت أنظر فرفع رأسه فقال ما لك يا عبد الرحمن قال فذكرت ذلك له فقال إن جبريل عليه السلام قال لي ألا أبشرك إن الله عز وجل يقول لك من صلى عليك صليت عليه ومن سلم عليك سلمت عليه (مسند أحمد، الرقم: ١٦٦٢، وقال البيهقي في الخلافيات ٣/١٤٣ عن طريق لهذه الرواية بنحو هذه الألفاظ :قال أبو عبد الله – رحمه الله -: هذا حديث صحيح)

Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu ‘anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alifanya sajda ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu (subhaanahu wata’aala) tayari amesha mchukuwa. Nilienda mbele yake kuangalia kuna kitu gani kimemkuta nabii wa mwenyezi mungu (sallallahu ‘alaihi wassallam). Kisha nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) aliinuwa kichwa chake cha baraka kutoka sajda na aliniuliza kuna tatizo gani, nikamueleza ni khofu yangu juu yako (yaani kutangulia mbele za haq ukiwa kwenye sajda). Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alisema, “(sababu ya kufanya sajida ndefu ilikuwa) jibraeel (alaihis salaam) alikuja kwangu na kusema, ‘je! nikupe bashara nzuri allah subhaana wata’alah alivyosema, ‘ yoyote atakae kusalia yaani kumsalia nabii, nitatuma rehma zangu kwake, na yoyote atakae kutumia salaam, nitatuma utulivu na baraka juu yake huyo mtu.'”

Mahari Ya Aadam (alaihis Salaam)

Sheikh Abdul haq Dehlewi (rahimahullah) aliandika kwenye kitabu kinaitwa ” madaarij un nubuwwah” kuwa pindi Hawwa (alaihas salaam) alipo umbwa , Aadam (alaihis salaam) alitaka kunyoosha mkono wake kumgusa. Malaaika walisema ” kuwa na subra mpaka ufunge ndoa na umpe mahari yake” kisha Aadam (alaihis salaam) aliuliza kwani mahari ni nini?” Malaaika walimjibu ” mahari ni kumsalia nabii wa mwenyezi mungu (sallallahu ‘alaihi wassallam)” (kutokana na riwaya zingine , mahari yalikuwa kumsalia nabii wa mwenyezi mungu (sallallahu ‘alaihi wassallam) mara ishirini.) (Al-Qowlul Badee’ Pg. 132, Fazaaile Durood Pg. 155)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …