عن عبد الرحمن بن مريح الخولاني قال سمعت أبا قيس مولى عمرو بن العاص يقول: سمعت عبد الله بن عمرو يقول: من صلى على رسول الله صلى الله عليه وسلم صلاة صلى الله عليه وملائكته سبعين صلاة فليقل عبد من ذلك أو ليكثر (مسند أحمد، الرقم: ٦٦٠٥، وإسناده حسن وحكمه الرفع إذ لا مجال للإجتهاد فيه كما في القول البديع صـ ٢٣٧)
Sayyidina Abdullah Bin Amr Bin Aas (radhiyallahu ‘anhuma) alitowa ripoti, “Yoyote atakaye tuma salaam kwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) mara moja Allah subhaana wata’alah na malaika wake watamtumia rehma na baraka sabini juu yake kwa kumlipa salaam yake moja. Kwahivyo yoyote atakaye taka kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam). Na yoyote atakaye kuwa ataki kuzidisha kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) asizidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) (yaani kama anataka kupata ujira mwingi,ni lazima azidishe kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam)).
Kumsaliya Nabii (Sallallahu ‘Alaihi Wassallam) Mara Nyingi Kuna Leta Msamaha Wa Allah Ta’alah
Sheikh Ibnu Hajar Makki (rahimahullah) alitowa ripoti kuwa mchamungu moja aliwahi kuonekana kwenye ndoto baada ya kufa kwake. Aliulizwa kuhusu hali yake katika akhera. Mchamungu alijibu, “Allah subhaana wata’alah alikuwa na rehma juu yangu, amesamehe madhambi yangu, na ameniingiza peponi” pindi alipokuwa ameulizwa sababu ya hivyo alijibu, ” malaika waliamrishwa kuyahesabu madhambi zangu na idadi ya kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam). Pindi zilivyonekana kuwa idadi ya kumsaliya Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) zinazidi madhambi zangu, Allah subhaaba wata’alah aliwaambia malaika na akasema, ” hii inatosha (kwa kumsamehe). Basi hesabu zaidi isiendelee. Mleteni muingize peponi.”””