Kupata Qiraat Moja Ya Thawabu

عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: من صلى علي صلاة كتب الله له قيراطا والقيراط مثل أحد (مصنف عبد الرزاق، الرقم: ١٥٣، وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٦٠)

Sayyidina Ali Bin Abii Taalib (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “yoyote atakae niswalia mara moja, Allah subhaana wata’alah atamuandikia kirati moja ya thawabu, na kirati moja ni sawa na mlima wa uhudi.

Kisa Cha Sura Kubadilika Rangi

Ndani ya Ihyaa Ul Uloomidin (kitabu), Imam Ghazaali (rahimahullah) anatoa kisa hiki kama jinsi Abdul Waahid Bin Zaid Basri (rahimahullah) alivyoeleza kwamba anasema: siku moja nilienda kuhiji. Mtu fulani alisafiri na mimi kama msafiri mwenzangu. Muda wote, wakati anatembea, akikaa, akisimama, aliendelea kumsalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam). Kisha nikamuliza sababu ya kumsalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) kwa wingi. Hakajibu:

Pindi nilipo hiji hija ya kwanza, baba yangu alisafiri na mimi. Pindi tulirudi, tulifika sehemu moja ya kupumzika na tukalala hapo. Wakati tulipokuwa pale, niliona ndoto mtu mmoja akiniambia, ” hamka, baba yako amefariki na sura yake imebadilika na kuwe nyeusi. Nikaamka na wasi wasi mwingi. Pindi nilipo mfunua nguo kwenye sura ya baba yangu, niligunduwa imebadilika na kuwa nyeusi. Hii imenifanya niwe na uzuni na hofu imenijia.

Nikalala na nikaota kwamba watu wanne wenye ngozi nyeusi na cheni za chuma, wanataka kumuadhibu, wamekaa pembeni mwa kichwa chake. Wakati huo mwanaume mzuri ambaye amevaa nguo mbili za kijani kapita na kuwafukuza hao watu wa nne. Alafu alipitisha mkono wake kwenye sura ya baba yangu na hakaniambia, “inuka (na ufurai) kwa ajili ya Allah subhaana wata’alah amebadilisha rangi ya sura ya baba yako. Sasa hivi ipo nyeupe. Basi ni kamuambia kwa furaha nyingi, wazazi wangu watolewe kafara juu yako, wew ni nani? Akajibu, jina langu ni Muhammad (sallallahu ‘alaihi wassallam)” Tangu wakati huo, sijaacha kumsalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam). (Ihyaau Uloom Deen 504/4)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …