Kupata Ukaribu Maalumu Wa Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) Siku Ya Kiama

عن عبد الله بن مسعود أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: أولى الناس بي يوم القيامة أكثرهم علي صلاة (سنن الترمذي، الرقم: ٤٨٤، وحسنه الإمام الترمذي رحمه الله)

Sayyidina Abdullah Bin Mas’ood (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah(sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema “mtu ambaye atake kuwa karibu sana na mimi (ambae anastahili sana msamaha wangu) siku ya kiama ni yule ambae alikuwa ananiswalia sana duniani.”

Sura Imebadilika Kuwa Kama Nguruwe

Katika nuzhatul majalisi, kisa kinachofuata kimerikodiwa: mtu na mtoto wake walikuwa kwenye safari. Njiani, baba kafariki na sura yake imebadilika kama nguruwe, mtoto kuona hili, alilia kwa uchungu na kuomba dua kwa Allah subhaana wata’alah kwa ajili ya baba yake.

Haikupita muda mtoto usingizi ulimpitia na hakaona mtu anamuambia, “baba yako alikuwa anakula riba, kwa sababu hii ndo unaona sura yake imekuwa katika hali hii. Lakin kuwa na furaha kwa sababu Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amemuombea msamaha kwa niaba yake, kila akisikia jina la Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) anamswalia. Kupitia msamaha wa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) sura yake imerudi katika hali yake ya kawaida.” (Nuzhatul Majaalis 82/2)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …