Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Pili

6. Sukutuwa mdomo na weka maji puwani kwa pamoja mara tatu.

Njia ya kusukutua mdomo na upandishaji wa maji puani ni ifuatayo: kwanza, chukuwa maji katika kiganja cha mkono wa kulia. Alafu tumia baadhi ya maji, sukutua mara moja. Baada ya hapo tumia yaliyobaki kiganjani pandisha maji puani. Hii njia utairudia mara mbili, kwa kutumia kiganja kingine cha maji kila mara.

Hakikisha unasukutuwa vizuri, kwa kuruhusu maji yafike sehemu zote mdomoni.[1]

عن وهيب عن عمرو عن أبيه شهدت عمرو بن أبي حسن سأل عبد الله بن زيد رضي الله عنه عن وضوء النبي صلى الله عليه وسلم فدعا بتور من ماء فتوضأ لهم وضوء النبي صلى الله عليه وسلم فأكفأ على يده من التور فغسل يديه ثلاثا ثم أدخل يديه في التور فمضمض واستنشق واستنثر ثلاث غرفات (صحيح البخاري، الرقم: 186)

Sayyidina Abdullah Bin Zaid (radhiyallahu ‘anhu) aliulizwa kuhusu udhu wa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) kwa hivyo aliomba kopo la maji liletwe. Alafu aliwaonyesha jinsi gani Nabii wa Allah alivyokuwa anafanya udhu. Alimimina maji mikononi mwake kutoka kwenye kopo la maji alafu akaosha mikono yake (mpaka kwenye vifundo) mara tatu. Baada ya hapo hakaingiza mikono yake kwenye kopo la maji na (kuchukuwa maji na) kusukutua mdomo wake na hakapandisha maji puani mara tatu.

7. Kama kuna haja ya kusafisha pua fanya hivyo kwa kutumia kidole cha mwisho cha mkono wa kushoto.[2]

عن أبى هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال إذا توضأ أحدكم فليستنشق بمنخريه من الماء ثم لينتثر (صحيح مسلم، الرقم: 237)

Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “mmoja kati yenu anapofanya udhu apandishe maji puani na baada ya hapo asafishe pua (kwa kutumia mkono wa kushoto).

8. Ukiwa na swaumu, kuwa makini kusukutuwa mdomo na kupandisha maji puani. Usizidishe kufanya hivyo, kwa sababu kuna uwezekano wa maji kuingia kwenye koromeo au mishipa ya pua, kwa hivyo inasababisha swaumu kuharibika.[3]

عن لقيط بن صبرة رضي الله عنه قلت يا رسول الله صلى الله عليه وسلم أخبرني عن الوضوء قال أسبغ الوضوء وخلل بين الأصابع وبالغ فى الاستنشاق إلا أن تكون صائما (سنن الترمذي، الرقم: 788)[4]

Sayyidina Laqeet Bin Sabirah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti “siku moja nimemuuliza Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) kuhusu udhu. Nabii wa Allah alisema, fanya udhu uliyokamilika, hakikisha unafanya khilaali ya vidole na pandisha maji puani vizuri, isipokuwa ukiwa na swaumu.””


[1] والصحيح بل الصواب تفضيل الجمع للأحاديث الصحيحة المتظاهرة فيه كما سبق وليس لها معارض … وفي كيفية الجمع وجهان أصحهما بثلاث غرفات ياخذ غرفة تمضمض منها ثم يستنشق منها ثم يأخذ غرفة ثانية يفعل بها كذلك ثم ثالثة (المجموع شرح المهذب 1/198)

قال الشافعي في المختصر يستحب أن يأخذ الماء للمضمضة بيده اليمنى واتفق الأصحاب على استحباب ذلك (المجموع شرح المهذب 1/198)

والمبالغة في المضمضة أن يبلغ الماء إلى أقصى الحنك ووجهي الأسنان واللثات ويسن إمرار إصبع يده اليسرى على ذلك، وفي الاستنشاق أن يصعد الماء بالنفس إلى الخيشوم، ويسن إدارة الماء في الفم ومجه وكذا الاستنثار (مغني المحتاج 1/171)

[2] وعن عائشة رضي الله عنها قالت كانت يد رسول الله صلى الله عليه وسلم اليمنى لطهوره وطعامه وكانت يده اليسرى لخلائه وما كان من أذى (سنن أبي داود، الرقم: 33)

قال أصحابنا ويستنثر بيده اليسرى (المجموع شرح المهذب 1/198)

ويسن … وكذا الاستنثار … وهو أن يخرج بعد الاستنشاق ما في أنفه من ماء وأذى بخنصر يده اليسرى (مغني المحتاج 1/171)

[3] وإن كان صائما رفق بالاستنشاق لئلا يدخل رأسه (الأم للإمام الشافعي رحمه الله 1/39)

[4] قال أبو عيسى: هذا حديث حسن صحيح

سنن أبي داود، الرقم: 142

About admin

Check Also

Njia Za Suna Za Kufanya Udhu – Sehemu Ya Tano

15. Fanya masaha ya masikio mara tatu na maji mengine. Pindi unapofanya masaha, tumia kidole cha shahada kufanya masaha ndani ya sikio na tumia kidole gumba kufanya masaha nje ya sikio (nyuma ya sikio). Baada ya hapo chukua maji mengine na ulowanishe kidole cha mwisho au kidole cha shahada. Alafu ingiza kidole cha mwisho au kidole cha shahada ndani ya sikio ili ufanye masaha ndani. Mwisho weka viganja vilivyolowa kwenye masikio.