عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال صلوا علي فإنها زكاة لكم واسألوا الله لي الوسيلة فإنها درجة في أعلى الجنة لا ينالها إلا رجل وأرجو أن أكون أنا هو (مسند أحمد، الرقم: 8770، وفي مجمع الزوائد (الرقم: 1877): رواه البزار وفيه داود بن علبة ضعفه ابن معين والنسائي وغيرهما ووثقه ابن نمير وقال موسى بن داود الضبي: حدثنا داود بن علبة وأثنى عليه خيرا وقال ابن عدي: هو في جملة الضعفاء ممن يكتب حديثه)
Abuu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema, “nisalieni kwa hakika ni njia ya usafishaji wenu. Muulize Allah subhaana wata’alah anijalie daraja la “waswila” ambayo ni daraja la juu la peponi limehifadhiwa kwa mtu mmoja tu, na ninamatumaini yangu kwamba mimi ni yule ambaye amebarikiwa na hii heshima na daraja.
Usalama Kutoka Kwenye Usumbufu Wa Kifo Kwa Ajili Ya Kumsalia Nabii Wa Allah Mara Nyingi
Ndani ya “nuzhatul majaalis” kisa kifuatacho kimeandikwa: siku moja, kuna mtu alimtembelea mtu ambaye anaumwa sana wakati alikuwa maututi, alimuuliza mgonjwa, “unaonaje uchungu wa mauti kwa wakati huu kwa kuiaga dunia?” Alijibu, “sisikii usumbufu wowote. Nimesikia masheikh wanasema yoyote anae msalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wassallam) kwa wingi atajikuta amesalimika kwa usumbufu wa mauti wakati wa kufa.” (Fazaaile Durood #181)