Tafseer

Tafseer Ya Surah Humazah

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ‎﴿١﴾‏ الَّذِى جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُۥ ‎﴿٢﴾‏ يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ اَخْلَدَهُ ‎﴿٣﴾‏ كَلَّا لَيُنْبَذَنَّ فِى الْحُطَمَةِ ‎﴿٤﴾‏ وَمَآ اَدْرٰىكَ مَا الْحُطَمَةُ ‎﴿٥﴾‏ نَارُ اللّٰهِ ٱلْمُوقَدَةُ ‎﴿٦﴾‏ الَّتِى تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْـِٔدَةِ ‎﴿٧﴾‏ اِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ ‎﴿٨﴾‏ فِى عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍ ‎﴿٩﴾‏ Ole wake kila msengenyaji, mdhihaki, aliye kusanya mali na kuendelea kuzihesabu! Anadhani kuwa mali yake itamfanya abakie milele. Kamwe! Hakika atatupwa katika ‘Hutamah’ (moto …

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah ‘Asr

بسمِ اللَّهِ ألرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ وَالْعَصْرِ ‎﴿١﴾‏ اِنَّ الْاِنسَانَ لَفِى خُسْرٍ ‎﴿٢﴾‏ إِلَّا الَّذِينَ اٰمَنُوْا وَعَمِلُوْا الصّٰلِحٰتِ وَتَوَاصَوْا بالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بالصَّبْرِ ‎﴿٣﴾‏ Naapa kwa zama; Hakika mwanaadamu yumo katika khasara, isipokuwa wale walio amini na wakatenda mema, na wakausiana na haki, na wakausiana kustahamili. وَالْعَصْرِ ‎﴿١﴾‏ اِنَّ الْاِنسَانَ لَفِى خُسْرٍ ‎﴿٢﴾ …

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah Takaathur

Kushindana baina ya watu katika kukusanya mali (na manufaa ya dunia) kumekushughulisha (kutoka katika utiifu wa Allah Ta‘ala na Akhera). (Hili linaendelea) mpaka mtazuru makaburi (yaani mpaka mtakapofariki). Hapana! hivi karibuni mtakuja kujua (ukweli wa mambo ya dunia ukilinganisha na Akhera, na malengo ya kweli ambayo mlipaswa kuyapigania). Tena, hivi karibuni mtakuja kujua (ukweli). Hapana! Lau mngelijua kwa ujuzi wa yakini (basi msingefanya hivi). Bila ya shaka mtaliona Moto wa Jahannam. Kisha bila ya shaka mtaliona kwa jicho la yakini. Kisha bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo (Siku ya Qiyaamah), kuhusu neema zote (mlizozistarehesha duniani).

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah Al-Qaar’iah

Siku ya tukio la Mpigiko; na ni siku gani ya tukio la Mpigiko? Na nini kitakujulisha kuhusiana na tukio la Mpigiko? Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa. Basi ambaye mizani yake (ya amali) ni nzito, atakuwa katika maisha ya furaha. Na ama yule ambaye mizani yake ni nyepesi, makazi yake yatakuwa “Haawiyah” (shimo la Jahannam). Na nini kitacho kujulisha nini hiyo? (Ni) moto mkali.

 

Soma Zaidi »

Tafseer Ya Surah ‘Aadiyaat.

(Naapa) kwa wale (farasi) waendao mbio kwa kuhema kwa pumzi, Na wakitengeneza cheche kwa kuzipiga (kwato zao) kwenye ardhi ya mawe (wanapokimbia), Na wakishambulia alfajiri, Na wakitimua vumbi nalo, Na wakijituma kati ya maadui. Hakika mwanadamu ni mwenye kumkufuru sana Mola wake. Na yeye ni shahidi wa ukweli huu. Na katika upendo wake wa mali, yeye ni mkali sana. Je, basi hajui (yatakayotokea) yatakapopinduliwa vilivyomo makaburini? Na yote yaliyomo ndani ya vifua (nyoyo) yatadhihirika. Hakika Mola wako siku hiyo atakuwa na habari zao zote.

Soma Zaidi »

Tafseer ya Surah Zilzaal

Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemesho wake. Na ardhi itakapotoa mizigo yake yote. Na watu watasema: Kumetokea nini? Siku hiyo itasimulia habari zake zote, kwa sababu Mola wako atakuwa ameiamrisha. Siku hiyo watu watarejea (kutoka mahali pa kuhesabiwa) makundi mbali mbali, ili waonyeshwe (matunda ya) matendo yao meema. Basi anayefanya jambo jema (hata) kwa uzito wa chembe, ataliona. Na anayefanya uovu (hata) kwa uzito wa chembe, atauona.

Soma Zaidi »

Tafseer ya Surah Bayyinah

بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ لَمْ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ ‎﴿١﴾‏ رَسُولٌ مِّنَ ٱللَّهِ يَتْلُوا صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ‎﴿٢﴾‏ فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ‎﴿٣﴾‏ وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوْا ٱلْكِتٰبَ إِلَّا مِن م بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ ‎﴿٤﴾‏ وَمَآ أُمِرُوٓا إِلَّا لِيَعْبُدُوْا ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُوْا ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُوْا …

Soma Zaidi »

Tafseer ya Surah Qadr

بِسمِ اللّٰـهِ الرَّحمٰنِ الرَّحيمِ اِنَّا أَنزَلنٰهُ فى لَيْلَةِ القَدْرِ ﴿١﴾ وَما أَدرىٰكَ ما لَيلَةُ القَدرِ ﴿٢﴾ لَيلَةُ القَدرِ خَيرٌ مِن أَلفِ شَهرٍ ﴿٣﴾ تَنَزَّلُ المَلـٰئِكَةُ وَالرّوحُ فيها بِإِذنِ رَبِّهِم مِن كُلِّ أَمرٍ ﴿٤﴾ سَلـٰمٌ هِىَ حَتّىٰ مَطلَعِ الفَجرِ ﴿٥﴾ Hakika Sisi tuliiteremsha (Qur’an) katika usiku wa Qadar (usiku wenye heshma kubwa). Na jambo gani  litakalokujulisha ni nini usiku wa …

Soma Zaidi »

Tafseer ya surah ‘Alaq

Soma kwa jina la mola wako ambaye ameumba (kila kitu). Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, na mola wako ni Mwingi wa Rehema. Ambaye amemfundisha (mwanadamu) kwa njia ya kalamu. Alimfundisha mwanadamu asiyoyajua. Kwa hakika, mwanadamu amekiuka mipaka yote, kwa sababu anajiona kuwa yuko huru. Hakika marejeo ni kwa Mola wako. Je, umemuona (Abu Jahl) ambaye anamsmamisha, mja (Muhammad (Sallallahu 'alaihi wasallam)) anaposimama katika Swalaah? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (mja - Muhammad (Sallallahu 'alaihi wasallam)) yuko juu ya uongofu, au anaamrisha kwa uchamungu (basi vipi Abu Jahl atamzuia)? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (Abu Jahl) atakataa na akageuka - hatambui kwamba Allah Ta’ala anaona kila kitu? Bali ikiwa (Abu Jahl) hataacha (maovu yake), tutamburuta kwa kisogo, kisogo cha uwongo mpotovu. Basi na aliite baraza lake, nasi tutaliita jeshi letu maalumu (la Malaika). Hapana! .Usimtii yeye (Ewe Muhammad (Sallallahu 'alaihi wasallam)), na uwe una sujudu na ukaribie (kwa Allah Ta’ala).

Soma Zaidi »

Surah ya Teen

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾ وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾ وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾ لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾ ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾ فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾ أَلَيْسَ اللّٰـهُ بِاَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾ Na aapa kwa mtini na mzeituni; na kwa Mlima wa …

Soma Zaidi »