(Naapa) kwa wale (farasi) waendao mbio kwa kuhema kwa pumzi, Na wakitengeneza cheche kwa kuzipiga (kwato zao) kwenye ardhi ya mawe (wanapokimbia), Na wakishambulia alfajiri, Na wakitimua vumbi nalo, Na wakijituma kati ya maadui. Hakika mwanadamu ni mwenye kumkufuru sana Mola wake. Na yeye ni shahidi wa ukweli huu. Na katika upendo wake wa mali, yeye ni mkali sana. Je, basi hajui (yatakayotokea) yatakapopinduliwa vilivyomo makaburini? Na yote yaliyomo ndani ya vifua (nyoyo) yatadhihirika. Hakika Mola wako siku hiyo atakuwa na habari zao zote.
Soma Zaidi »Salaa na Salaam Ma’luum ya Ibn Abbas (radhiyallahu ‘anhuma)
عن ابن عباس أنه كان يقول: اللهم تقبل شفاعة محمد الكبرى وارفع درجته العليا وآته سؤله في الآخرة والأولى كما آتيت إبراهيم وموسى (مصنف عبد الرزاق، الرقم: 3104، وإسناده جيد قوي صحيح كما في القول البديع صـ 122) Ibn Abbas (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba alipokuwa akimtumia salaa na salaam juu …
Soma Zaidi »Sunna Za Msikiti
7. Ingia msikitini kwa mguu wa kulia.
Imepokewa kwamba Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) amesema, “Imetoka kwenye Sunna kwamba unapoingia msikitini uingie kwa mguu wako wa kulia, na unapotoka msikitini utoke kwa mguu wako wa kushoto.
Soma Zaidi »Salaa na Salaam Maalum ya Ibnu Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu)
Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) Anaeleza, “Unapomswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), basi mswalie kwa adabu bora zaidi (yaani kwa kujitolea, umakini, upendo na heshima), kwa hakika wewe hujui ya kwamba huenda hio salaa na salaam zenu zitahudhurishwa mbele yake. Wanafunzi wa Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) waliuliza, “Tufundishe jinsi ya kutuma salaa na Salaam juu ya Rasulullah sallallahu alaihi wasallam ” Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Soma yafuatayo:
Soma Zaidi »Sunna Na Adabu Za Kuchinja – Sehemu ya 4
18. Mtu asianze kumchuna mnyama huyo mpaka kusiwe na dalili ya uhai iliyosalia katika mwili. 19. Wakati wa kuchinja mtu asome tasmiyah kwa namna ifuatayo: بِسمِ اللهِ اللهُ أكْبَر Kwa jina la Allah Ta’ala, na Allah Ta’ala ndiye mkubwa zaidi. 20. Kabla ya kuchinja ni sunna kwa mtu kusoma dua …
Soma Zaidi »Sunna na Adabu za Kuchinja – Sehemu ya 3-
11. Ikiwa mtu ana uwezo, ni bora kwake kuchinja mnyama mwenyewe. Ikiwa hili haliwezekani, basi angalau ashuhudie mnyama wake akichinjwa, mradi tu hijaab inazingatiwa kati ya wanaume na wanawake (yaani kuingiliana kusifanyike). عن علي رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم قال يا فاطمة قومي فاشهدي …
Soma Zaidi »Tafseer ya Surah Zilzaal
Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemesho wake. Na ardhi itakapotoa mizigo yake yote. Na watu watasema: Kumetokea nini? Siku hiyo itasimulia habari zake zote, kwa sababu Mola wako atakuwa ameiamrisha. Siku hiyo watu watarejea (kutoka mahali pa kuhesabiwa) makundi mbali mbali, ili waonyeshwe (matunda ya) matendo yao meema. Basi anayefanya jambo jema (hata) kwa uzito wa chembe, ataliona. Na anayefanya uovu (hata) kwa uzito wa chembe, atauona.
Soma Zaidi »Salaa na Salaam ya Ibrahim (‘alahi salaam)
Abdur Rahmaan bin Abi Laila (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti:
Ka’b bin Ujrah (radhiyallahu ‘anhu) aliwahi kukutana nami na kuniuliza, “Je! nikupe zawadi niliyoipata kutoka kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)? Nilijibu, “Ndiyo, kwa kweli tafadhali nipe hiyo zawadi.” Alisema, "Wakati mmoja, tulimuuliza Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ‘Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), ni Namna gani kukutumia wewe na familia yako salaa na salaam, hakika Allah ta'ala ametufundisha (kupitia kwako) jinsi ya kukutumia salaa na salamu?’” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Sema.
Soma Zaidi »Sunna na Adabu za Kuchinja – Sehemu ya 2-
6. Ni sunna kwa mtu kujiepusha na kula chochote asubuhi wa Idul Adha (idi kubwa) mpaka arudi kutoka katika swala ya Idi. عن ابن بريدة عن أبيه رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه و سلم كان لا يخرج يوم الفطر حتى يأكل . وكان لا يأكل يوم …
Soma Zaidi »Kumswalia Nabii wa Allah sallallahu alaihi wasallam katika Maeneo ambayo Watu wameghafilika.
Abu Waa’il (rahimahullah) anaeleza, “Sijawahi kumuona Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) akihudhuria mkusanyiko au mwaliko wowote, isipokuwa tu kwamba angemhimidi na kumtukuza Allah subhaana wata'ala na kumtumia salaa na salaam juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kama ingemlazimu kwenda sokoni, ambako alikuta watu wameghafilika na kumkumbuka Allah ta'ala, basi angemhimidi Allah ta'ala Na kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika sehemu hizo.”
Soma Zaidi »