Kupata Uombezi Na Bashara wa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن ابن عمر قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من زار قبري وجبت له شفاعتي (سنن الدارقطني، الرقم: 2695) رواه البزار والدارقطني قاله النووي وقال ابن حجر في شرح المناسك: رواه ابن خزيمة في صحيحه وصححه جماعة كعبد الحق والتقي السبكي وقال القاري في شرح الشفا : صححه جماعة من أئمة الحديث. (فضائلِ حج صـ 182)

Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Yoyote anayezuru kaburi langu, uombezi wangu unakuwa lazima kwake (yaani kwa hakika nitamuombea kwa Allah Ta’ala siku ya Qiyaamah kumsamehe mtu huyo).

Njia ya kupata ukaribu wa Allah subhaana wata’alah

Ka’b Ahbaar (rahimahullah) (ni taab’ iee ambaye alikuwa miongoni mwa wasomi wa mayahudi aliyekubali uislaam) ameripoti:

Allah subhaana wata’alah alimuambia Moosa (alayhis salaam) kwa kusema, ewe Moosa, Unatamani kuwa karibu nami, kuliko maneno yako yalivyo karibu na ulimi wako, au karibu zaidi kuliko hisia zako za ndani zilivyo na moyo wako, au karibu zaidi kuliko nafsi yako ilivyo kwa mwili wako, au karibu zaidi kuliko maoni yako yalivyo karibu na macho yako? “Moosa (alayhis salaam) alijibu kwa kusema ndio. Allah subhaana wata’alah kisha alisema, basi soma salaamu kwa wingi kwa Muhammad (sallallahu alaih wasallam).” (Al-Qawlul Badee, Pg,270)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …