Usiku Ukisubiri Muda Maalum Wa Kisomo

Katika riwaya moja, imepokewa kwamba kila mtu aliyejifunza Qur-aan Takatifu (au kipande chake) anaposimama katika Swalaah
kwa Muda mchache usiku, ili asome Qur-aan, basi usiku huo unaujulisha usiku unaofuata juu ya nyakati hizi maalum ambazo ulikuwa umeufurahiya. Usiku unaushawishi usiku unaofuata kungojea kwa hamu nyakati hizo maalum ambapo utasimama kusoma Qur-aan katika Swalaah. Usiku huo pia unauomba usiku unaofuata kuwa mwema kwa huyo mtu.[1]

Baraka Za Qur-aan Zinatiririka Baada Ya Mtu Kufariki

Kama vile baraka za Qur-aan tukufu zinavyofurahiwa hapa duniani, basi hivyo ndivyo baraka za Qur-aan tukufu zitaendelea kumbariki katika maisha ya baadae. Quran Takatifu inamnufaisha mtu kaburini na Akhera, mpaka itamwingiza Peponi.

Imepokewa katika riwaya kwamba mtu ambaye aliendelea kujitolea kwa Quraan Takatifu wakati wa uhai wake, basi pindi atakapofariki paa ya nuru iliyokuwa ikiifunika nyumba yake wakati wa uhai wake itainuliwa kutoka kwenye ardhi. Hivyo, Malaika watakuwa wakitazama hiyo nuru mbinguni lakini hawataiyona hiyo nuru.

“Baada ya kuaga dunia, na nuru yake inapoenda mbinguni (kukutana na Allah Ta’ala), Malaika wa kila mbingu hukutana naye, na katika nafsi zote humridhia yeye na kumuombea dua maalum. Kisha anakutana na wale malaika ambao walikuwa wakibaki naye katika maisha yake yote, wakimlinda na madhara, na wao pamoja na Malaika wengine humuombea dua ya maghfirah mpaka siku ya Qiyaamah.[2]


[1] ورواه ابن أبي الدنيا وغيره عن عبادة بن الصامت موقوفا عليه ولعله أشبه كذا في الترغيب والترهيب للمنذري 1/ 245

[2] ورواه ابن أبي الدنيا وغيره عن عبادة بن الصامت موقوفا عليه ولعله أشبه كذا في الترغيب والترهيب للمنذري 1/ 245

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "