Kusoma Quraan Takatifu

Allah Ta’ala amebariki Umma wa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na bahari isiyo na mwisho. Bahari hii imejaa na lulu, zumaridi, na marijani (Aina tofauti za majiwe ya thamani). Kwa kadri mtu atakavyochota kutoka kwenye bahari hii, ndivyo mtu atafaidika zaidi. Bahari hii haitoisha kamwe bali itaendelea kubariki mtu katika dunia hii na ijayo. Bahari hii isiyo na mwisho ndio Quraan Tukufu.

Quraan Takatifu ni fadhila kubwa kabisa ya Allah Ta’ala juu ya Ummah huu. Ni maneno ya Allah Ta’ala kwa viumbe vyake na hakuna fadhila yoyote duniani inayoweza kuwa sawa sawa nayo.

Kama tu Ummah huu utaushikilia Quraan Takatifu kwa uthabiti na kutimiza haki zake, itakuwa ni chanzo cha nuru kwao hapa duniani na kaburini. Zaidi ya hayo, Siku ya Qiyaamah, itawashindikiza kwenye uwanja wa Qiyaamah mpaka itawaingiza Peponi.

Nyumba ambayo Qur-aan inasomwa ndani yake

Katika Hadith, imetajwa kwamba nyumba ambayo Qur-aan Takatifu inasomwa ndani yake ina baraka ambazo Malaika hukusanyika humo na rahma maalum za Allah Ta’ala huteremka juu yake.

Imepokewa katika riwaya ya Ubaadah bin Saamit: “Nyumba ambayo Quraan inasomwa ndani yake imefunikwa na paa ya nuru ambayo Malaika wa mbinguni wanautafuta mwelekeo na mwanga wake kama vile meli inayosafiri katikati ya bahari au msafiri katika nchi kavu anavyotafuta mwelekeo na nuru kupitia nyota inayong’aa.”[1]

Katika Hadith nyingine, imepokewa kwamba nyumba ambayo Qur-aan Tukufu inasomwa ndani yake inasababisha baraka kuingia ndani ya famalia, Malaika wanateremka juu yao na mashetani kuondoka nyumbani humo, na wema kuongezeka nyumbani humo, lakini nyumba ambayo Quraan Tukufu haisomwi ndani yake, basi maisha yao yatakuwa magumu, Malaika wataondoka katika hiyo nyumba na mashetani watakaa humo na nyumba kama hiyo haitakuwa na baraka.”[2]


[1] ورواه ابن أبي الدنيا وغيره عن عبادة بن الصامت موقوفا عليه ولعله أشبه كذا في الترغيب والترهيب للمنذري 1/ 245

[2] سنن الدارمي، الرقم: 3352، ورجاله رجال البخاري إلا معاذ بن هانئ وحفص بن عنان وكلاهما ثقة

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …