Wakati wa vita vya Badr, mtoto wa Abu Bakr Siddeeq (radhiya Allaahu ‘anhu), Abdur Rahmaan (Radhiyallahu ‘anhu), alipigana upande wa makafiri kwa vile alikuwa bado hajaukubali Uislamu.
Baadaye, baada ya kusilimu, akiwa amekaa pamoja na baba yake, Abu Bakr Siddeeq (Radhiya Allaahu ‘anhu), alisema, “Ewe baba yangu kipenzi, wakati wa vita vya Badr, uliingia chini ya upanga wangu mara chache. Hata hivyo, kwa kuwa wewe ni baba yangu, nilikuacha.”
Abu Bakr Siddiq (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijibu hapo hapo, “Lau wewe ungekuwa chini ya upanga wangu wakati wa vita, nisingekuacha kamwe Kwa sababu ulikuwa ukipigana kumpinga Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)”.