Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا مجالسكم بالصلاة علي فإن صلاتكم علي نور لكم يوم القيامة (الفردوس بمأثور الخطاب، الرقم: ٣٣٣٠، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٨)

Ibnu umar (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alisema, “Pamba mikusanyiko yenu na kunitumia salaam, kwa sababu siku ya qiyaama, salamu zenu juu yangu itakuwa nuru (sababu ya nuru) kwenu.”

Kufikisha salaa na salaam kwa niaba ya Mtu mwengine kwenye Kaburi la Rasulullah (sallallahu alaih wasallam)

Yazid bin Abi Said Al-Madani (rahimahullah) anataja:

Wakati mmoja (nikiwa na nia ya kusafiri kwenda Madinah Munawwarah), nilimuaga Umar bin Abdil Azeez (rahimahullah) Umar (radhiyallahu anhu) akaniambia, “Nina mahitaji ambayo nataka unitimizie.” Nikajibu, “Ewe Ameerul Mu’mineen! Unataka nifanye nini kutimiza?”

Akajibu: “Utakapofika Madinah Munawwarah na ukiona kaburi lililobarikiwa la Rasulullah (sallallahu alaih wasallam), Basi unifikishie salamu zangu kwa Rasulullah (sallallahu alaih wasallam).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …