Miaka Thamanini ya Kusamehewa madhambi, na Miaka Thamanini ya Ibaadah Inarikodiwa kwa kumswalia Nabii wa Allah Mara Thamanini kwenye siku ya Ijumaa

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى صلاة العصر من يوم الجمعة فقال قبل أن يقوم من مكانه اللهم صل على محمد النبي الأمي وعلى آله وسلم تسليما غفرت له ذنوب ثمانين عاما وكتبت له عبادة ثمانين سنة (القول البديع صـ 399)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kuswali Swalah ya Al-Asiri siku ya Ijumaa na kisha akatuma salaa na salaam ifuatayo mara thamanini kabla ya kusimama kutoka mahali pake, atasamehewa miaka thamanini ya madhambi na miaka thamanini ya ibaadah (nafl) atandikiwa:

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ وَعَلٰى آلِهِ وَسَلِّمْ تَسْلِيْمًا

Ewe Allah, tuma salaa na salaam tele juu ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) Nabii asiye jua kusoma, na juu ya familia yake.

 

Fadhila za Kuzuru Raudhah Mubaarak (Kaburi la Rasulullah Sallallaahu ‘alaihi wasallam) ya Mtume wa Allah Ta’ala

Muhadith mashuhuri wa madhehebu ya kihanafi, Mulla Ali Qaari (rahimahullah), ameandika kwamba kuna makubaliano baina ya Maaulama kwamba kuzuru kaburi la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ni kitendo muhimu cha wema na pia kitendo cha uchamungu, na ni aina ya ibaadah inayotamanika sana, pia ni njia ya mafaanikio kupata kuinuliwa kiroho na sababu ya kupata uombezi wa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

Baadhi ya Maulamaa wametaja kuwa ni waajib kwa mwenye uwezo kufika Madina Munawwarah. Mwanasheria mashuhuri, Allaamah Shaami (Rahimahullah), amenukuu maoni haya kutoka kwa Haafidh Ibnu Hajar (rahimahullah), kwamba kuto kwenda Madinah Munawwarah ni kitendo cha uzembe na kutokujali kabisa.

Kwa kuzingatia ihsani kubwa za Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) juu ya Ummah huu, ni haki yake kuzuru kaburi lake la baraka kama utakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kwa hakika ni kitendo chu kusikitisha ikiwa mtu atasafiri kwenda kuhiji au kufanya umrah, na licha ya hayo akiwa na uwezo, lakini baado hatembelei kaburi la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Kuna makubaliano miongoni mwa madhehebu manne kwamba ni mustahab kuzuru kaburi la Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …