Mtu wa Kwanza katika Ummah huu kuingia Jannah

Katika Hadith, Rasulullah (sallallaahu ‘alaihi wasallam) ameeleza kwamba Ummah wake utaingia Jannah kabla ya Ummah wote wengine, na katika Ummah wake wote, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) atakuwa mtu wa kwanza baada yake kuingia Jannah.

Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Jibreel (‘Alayhis Salaam) alikuja mbele yangu, akanichukua kwa mkono na akanionyesha mlango wa Jannah ambao Ummah wangu utaingilia.”

Abu Bakr (radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Natamani ningekuwa pamoja nawe (wakati Jibreel (‘alayhis salaam)) alipokuonyesha mlango wa Jannah) ili na mimi niuone!”

Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “kuhusu wewe, Abu Bakr, utakuwa mtu wa kwanza wa ummah wangu kuingia Jannah.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …